Zinazobamba

mwakyembe apimwa ubavu, soma hapa

waziri wa uchukuzi  DK harrison mwakyembe akifafanua jambo

Na Karoli Vinsent

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameingia katika mzani wa
kupimwa ubavu na uongozi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA)
ambao unasuasua kutekeleza agizo lake la kumtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa shirika hilo, Ronald Phiri, kutoendelea kuishi hotelini na badala yake
apewe nyumba ya kuishi ili kukwepa gharama pamoja na ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Ronald Phiri, kwa takriban miezi 6 sasa
anatajwa kuishi katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam kwa
gharama ya shirika hilo na hivyo kuteketeza mamilioni ya shilingi.

[image: New Africa Hotel]Habari zilizopatikana kutoka Ofisi za Makao Makuu
ya TAZARA, Dar es Salaam, zinadai kwamba phiri amekuwa akilipia chumba
anachokitumia kulala katika hoteli hiyo dola za Marekani 200 (takriban Sh
320,000) kwa siku, sawa na takriban Sh. 9,600,000 kwa mwezi. Kwa hesabu
hiyo, kwa miezi hiyo sita ambayo Khiri ameishi hotelini hapo, TAZARA
italipa Sh. 57,600,000.

Hasara yote hiyo kwa shirika la TAZARA inaingiwa wakati Waziri wa Uchukuzi,
Dk. Harrison Mwakyembe amemwagiza Kaimu Mkurugenzi huyo kuhamia katika
nyumba ya TAZARA iliyoko Masaki, ambayo ilikuwa ikitumiwa na mtangulizi
wake, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Akashambatwa Lewanika.

Lewanika alistaafu ajira yake mwanzoni mwa mwaka huu na kurejea nchini kwao
Zambia, kabla ya Bodi ya TAZARA kumteua Khiri kukaimu nafasi hiyo.

Akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA Oktoba 21, mwaka huu, Dk Mwakyembe
alimpa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo, Khiri, muda wa wiki mbili kuondoka
hotelini hapo na kuhamia katika nyumba ya shirika.

Mmoja wa wafanyakazi wa TAZARA ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia
kwenye Blogs hii akisema: “Unajua mpango wa kumweka hotelini (Phiri)
ulikuwa ni wa muda wa miezi mitatu tu, lakini kama ujuavyo gharama za
kuishi hotelini pale ni dola za Marekani 200 kwa siku.

Kwa hiyo, miezi mitatu imepita na sasa ni miezi zaidi ya sita.”

Akizungumzia hali hiyo ya kuendelea kuishi hotelini hapo kinyume cha
maelekezo ya Waziri Mwakyembe, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TAZARA anasema hata
yeye hajisikii raha kuishi hoteli hiyo ya New Africa, akisema hali hiyo
inamsababishia kuishi mbali na familia yake.


Khiri anasema: “Ni kweli niliambiwa niondoke hotelini hapa na waziri,
lakini mpaka sasa sijaondoka. Hata hivyo, hata mimi mwenyewe sijisikii
furaha kuishi hapa hotelini kwa sababu inanifanya niishi mbali na familia
yangu.

“Bodi ya TAZARA ilitakiwa ikutane mwezi Juni kwa ajili ya kujadili suala
langu. Lakini Mkurugenzi aliyekuwa akiishi katika nyumba ninayotakiwa
nihamie, bado hajaondoa samani zake, kwa hiyo ninachosubiri ni kikao cha
bodi kujadili hatima yangu.”

Kwa upande wake, Mwanasheria wa TAZARA, Marko Mabala, alipo ulizwa alisema:
“Hili suala lina mitazamo ya kisiasa na kiutendaji.

Dk Mwakyembe alitoa agizo aondoke hotelini, lakini nyumba anayotakiwa
kuhamia bado inashikiliwa na mkurugenzi aliyeondoka na hata funguo
ameondoka nazo Zambia.

“Kwa hiyo, ile nyumba imefungwa. Nilimwandikia notisi, akasema hahitaji
notisi, bali atakuwa tayari kuachia funguo za nyumba baada ya kulipwa mafao
yake yote.

“Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TAZARA aliyeondoka kushikilia
msimamo wake huo bado, upande wa Serikali ya Zambia unahoji ni kwa vipi
shinikizo la kuachia nyumba liwe kwa Akashambatwa pekee, ilihali aliyekuwa
Naibu Mkurugenzi wake, Ayoub Ritti anaishi nyumba ya TAZARA iliyoko maeneo
ya Kawe kwa muda wa miaka 15 sasa wakati si mfanyakazi wa TAZARA na halipii
pango la nyumba hiyo.

“Naulizwa maswali (Mabala), kwa nini unasema Akashambatwa aondoke wakati
hujamlipa haki zake zote, huku Ritti ambaye si mfanyakazi wa TAZARA
akiendelea kuishi katika nyumba za shirika wakati halipii pango?”

Ritti alikuwa mfanyakazi wa TAZARA, lakini alifutwa utumishi wa shirika
hilo tangu mwaka 1998 na hadi sasa hajaondoka katika nyumba aliyokuwa
akiishi na familia yake wakati alipokuwa Naibu Mkurugenzi.

Habari zinasema wengine wanaoidai TAZARA, ni pamoja na Damas Ndumbaro,
aliyekuwa Naibu Mkurugenzi huku Akashashamtwa ambaye kwa taarifa zilizopo
ndani ya shirika hilo, anadai dola za Marekani 108,000.

Habari hii imeandikwa na Karoli Vinsent kwa kushirikiana n Gazet la Raia
Mwema

Hakuna maoni