Zinazobamba

tuache unafiki uchumi wetu unategemea bomba la Mtwara, anayebisha anaajenda ya siri>>>>>>> PRO. SOSPETER MUHONGO AFUNGUKA

Waziri wa Nishati na madini amewataka watanzania kuunganisha nguvu zao kw pamoja kuhakikisha mladi wa ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara unakamilika kwa wakati ili Tanzania tuanze kufaidi matunda ya bomba hilo kuliko kupoteza wakati kwa kusema vibaya juu ya mradi huo ambao ndio chimbuko la kufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kipato cha kati

waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo akifafanua jambo kwa wadau wa madini mapema hii leo, Muhongo amewataka wadau hao kusoma sera za madini ili waelewe kwa makini na kuwa mabalozi wazuri wa serikali katika maeneo yao ya kazi
Profesa Muhongo ameenda mbele zaidi na kusema wale wote ambao wanadhani serikali kwa kuruhusu ujenzi wa bomba hilo wamekurupuka inapidi wajipime na kungalia wenzetu wa nchi jirani wanafanya nini katika harakati za kuinua uchumi wa nchi zao kwa kutumia rasilimali za madini na gesi,
Hayo ameyasema mapema hii leo wakati akizungumza na wadau tokamikoa 11 inayojishughulisha na uchimbaji wa madini na kuwaelewa pasipo kupepesa macho kuwa kuna haja ya watanzania hususani wale wanaotoka katika sehemu ambazo madini yanachimbwa, wasome kwa makini sera ya madini ya mwaka 2009 na wakaielewa ili waeze kujenga hoja wakati wanapodai haki zao

"Unakuta mtu anasema kuwa suala zima la kusaini mikataba ya madini ni siri au mtu anakurupuka anasema kuwa sera ya madini haipo na kwamba ndio maana tunapunjwa katika sualazima la gawio  na hao wawekezaji", hilo suala halipo kabisa katika uongozi wangu, ningependa watu wakafahamu kuwa suala la kusainiwa kwa mikataba ya madini sio siri hata kidogo na yeyote anayetaka kuisoma basi asisite kufanya hivyo.

Aidha Prof. Muhongo amebainisha wazi kuwa watanzania wengi hawapendi kusoma na wanapenda kusimuliwa zaidi, kufanya hivyo kunalemaza na kwamba yule mtu anayekusimulia anaweza akaongeza chumvi ili maslahi yake yaweze kufikiwa
Jamani nawaomba sana someni kwani kusoma kutawafanya muweze kujiamini na kuhoji maswali ambayo yataijenga nchi yetu

Mfano mzuri ni hilo bomba letu tunalolijenga toka huko mtwara likikamilika , nawahakikishieni kuwa tatizo la umeme katika nchi hii ni historia teanatena, tuacheni unafiki wa kusema vibaya miradi mizuri kama hii aliongeza .
wadau walioshiriki katika mkutano huo wa siku mbili wakimsikiliza kwa makini waziri Muhongo, wadau hao wametoka sehemu mbalimbali ya nchiyetu wakijumuisha mapadri na maasikofu pamoja na mashehe wakubwa kabisa


nakukaribisha muheshimiwa waziri.

tunasikiliza, wakiwa makini kabisa
Askofu medhodkiraini akifafanua jambo juu ya mustakabali mzima wa madini ,


Hakuna maoni