Zinazobamba

MNAZI MMOJA SASA BALAA, POSTA SHWAAAAAARI


 Abiria wakiwa wameteremka kutoka kwenye daladala katika Kituo cha Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo mchana, tayari baadhi yao kuanza safari kwa miguu kwenda eneo la Posta katikati ya Jiji hilo, kutokana na baadhi ya daladala kutoruhusiwa kufika Posta ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART). Ujenzi katika eneo la Posta na Feri unatarajia kukamilika baada ya miezi mitatu. Daladala zinazotakiwa kuishia Mnazi Mmoja ni kutoka Gongo la Mboto, Vingunuti, Temeke, Tabata, Segerea  na Buguruni
Posta Mpya Dar es Salaam, ikiwa haina daladala nyingi jioni ya leo saa 10, baada ya daladala za maeneo mengine jiji isipokuwa Mwenge, Ubungo, Mabibo na Mbezi kupigwa marufuku kufika  eneo hilo bali yaishie Mnazi Mmoja na Stesheni kuanzia leo, ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam DART.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)

Hakuna maoni