Kimenuka strabag, wafanyakazi , vibarua wagoma tena
Wafanyakazi wa kampuni ya strabag mapema hii leo wamegoma
kwenda kazini baada ya vibarua waliokuwa wakifanya kazi katika kampuni hiyo
kuhamishiwa kazi hiyo kwa mzabuni mpya pasipo taarifa rasmi ya kimaandishi,
Wakizungumza na mtandao huu, wafanyakazi hao, wamesema kuwa
wameamua kuacha kufanya kazi kwa siku hii ya leo baada ya kubaini kuwa vibarua
wa kampuni hiyo ya strabag wametimuliwa pasipo taarifa maalum,
Wamesema kuwa kampuni ya strabag wameingia mkataba na
kampuni ya Laba construction ili waweze kuajiri wafanyakazi wengine huku wao
wakiachwa solemba wasijue la kufanya
VIbarua hao wameishutumu kampuni ya kizalendo ya laba
construction kwa kitendo chao cha kuchukua tenda katika kampuni ya starabag na kuanza
kuwanyanyasa vibarua waliowakuta kwa kuwashushia mapato yao
kwa asilimia kubwa sana
KWA sasa kampuni ya Laba construction ltd imetangaza wazi
kuwa wako tayari kuwalipa wafanyakazi wote malipo ambayo sheria inawataka
kuwalipa na kwamba kinyume cha hapo hawako tayari kuongeza malipo yoyote
Yeyote atakayataka kufanya kazi na Laba construction na
afanye , kama mtu anaona haina maslahi basin a
achaane na kampuni akafanye kazi nyingine kwani kazi ziko nyingi, aliongeza
mkurugenzi wa kampuni ya strabag
Akizunguma na mwandishi wa habari hizi, mkurugenzi wa
kampuni iliyojikita katika suala zima la kuajiri viabarua katika sekta ya ujenzi wa mabarabara, Bw.
Emanuel Mshana amesema shutuma ambazo zinaelekezwa katiaka kampuni yake ki
msingi hazina mantiki, kwani sheria iko wazi kuwa katiaka sekta hiyo mshahara
wa vibarua unaanzia shilingi 9616 kwa kutwa huku kwa lisaa ni shilingi 1282
Taarifa ambazo mtandao huu zimelinisa ni kwamba kampuni ya
Laba construction imenyanyasa wafanyakazi waliowakuta na kuwafanya wengine
waanze kufikilia namna gain wataishi huku wengine wakilia kurudi katika kampuni
ya strabag ili walipwe salio lao la awali
VIBARUA WA STRABAG WAKIWA NJE YA OFISI YA STRABAG WAKIWA HAWAJUI LA KUFANYA, WAFANYAKAZI HAO WAMEGOMA BAADA YA KAZI ZAO KUPEWA WATU WENGINE |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni