Zinazobamba

Mhogo; Dhahabu nyeupe inayooza ardhini *linazalisha bidhaa zaidi ya 300 *bei ya unga ni dolla 2 kwa kg


 


 
Na Mobini Sarya,ANSAF
 
ZAO la mhogo ni miongoni mwa mazao yasiyopewa kipaumbele kikubwa hapa nchini,huku likibainika kuwa ni sawa na dhabu nyeupe inayooza ardhini.
 
Msimu wa kilimo unapowadia wakulima wengi huanza kufikilia kulima mahindi kama zao la chakula na biashara  kisha hufuatiwa na mazao mengine ya biashara, mhogo   ukionekana  kama la ziada katika baadhi ya mikoa.
 
Hata hivyo imebainika kuwa zao la mhogo licha ya kwamba linalimwa kwa wingi hapa nchini lakini faida yake haijaonekana kutokana na jnsi linavyoandaliwa na kusababisha mkulima kupata faida kidogo.
hivyo kama wazalishaji wa viwandani wakiamua kukaa na wakulima wakapeana elimu ya kusindika unga wa mhogo unaotakiwa kwenye viwanda vyao Tanzania inaweza kumaliza tatizo la njaa na umasikini kwa wakati mmoja.

zao hilo linaweza kushindana na madini ya dhahabu kama likitumika vizuri kwani lina utajiri wa ajira tangu linaandaliwa shambani hadi kuvunwa na kusindika unga wake ambao utazalisha bidhaa mbalimbali huku serikali ikipata kodi tafauti na ilivyo sasa ambapo serikali haipati chochote.

Hiyo ni kutokana na  utafiti uliofanyika nchini Italia kuhusiana na zao hilo na kuonyesha kuwa zao la muhogo linaweza kutumika kwa matumizi  mbalimbali zaidi ya 300 yakiwemo chakula na bidhaa kama tambi,bisukuti,mafuta ya lishe,keki,sabuni ya unga, kuni, mboga,huksi pamoja na bidhaa nyingine nyingi.
Matumizi yote yaliyotajwa yanatakikana hapa nchini na viwanda vyake vipo,lakini cha kusikitisha kama sio usaliti wa wenye viwanda hivyo wamekuwa wakiagiza unga huo kutoka nje ya nchi.
Lakini pia wakati zao hilo  kwa wananchi walio wengi  linachukuliwa kama zao la kinga ya njaa hali iliyosababisha  mikoa yenye chakula kingi kuliacha likiozoea shambani wakisubiri kipindi cha njaa imefahamika kuwa linaweza kumuingizia mkulima kipato cha haraka kama soko lake likitangazwa vizuri .
“Kikwazo kikubwa sio upatikanaji wa unga wake bali ni namna wanavyouandaa ili  sumu yake iweze kutoka ndani ya masaa 12 uwe umepatikana unga mweupe”anasema Julias Wambura ambaye ni msambaza wa nafaka kwenye masoko.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa Kilimo ulioandaliwa na Jukwaa la mkulima ANSAF, Mkurugenzi wa kampuni ya Frabho Enterprises, Julias Wambura anasema kuwa amepata soko la kuuza unga wa mhogo tani 400 kwa mwezi kwenda china lakini unga huo umekosekana.
 
“Soko la mhogo ni kubwa kuliko zao lolote hivi sasa  sema wakulima wetu hawajandaliwa…..mimi mwenyewe nimepata soko la kuuza unga huo  tani 400 kwa mwezi lakini umekosekana wachina waliniambia nikiweza watanilipa dolla 2 kwa kilo ambayo ni sawa na shilingi 3200”anasema Wambura
mihogo
 
Anasema katika utafiti wake amegundua kuwa Tanzania inalima tani Milioni 7 za mhogo kwa Mwaka hivyo kama wakulima wangeandaliwa vizuri na kupewa mashine ya kusindika unga wenye ubora Tanzania ingepiga hatua kubwa kimaendeleo kwasababu zao hilo linastawi haapa nchini na halihitaji gharama kubwa kulilima.
 
Wambura anasema kuwa nchini Nigeria Serikali ilitunga sheria kwamba ni laima kila anayekaanga mikate kiwandani achanganye na unga wa mhogo kama njia ya kulinda soko la unga wa mhogo na kuwapa wakulima  hamasa ya kuendelea kulima zao hilo.
Wakati zao limebainika kutumika kuzalisha bidhaa zaidi ya 300 nchini Tanzania katika Soko la Dar es Salaam,mhogo umebaki kuwa kitafunio cha chai pekee, au unaweza kuambulia kupata unga wake kwenye maduka makubwa ya supermarket hivyo kufanya soko lake kuwa dogo.
Hivyo wadau wanashauri serikali kuwapa elimu ya kusindika unga wa mhogo kwa teknojia ya kisasa na kuzuia uingizaji wa unga huo kutoka nje kwani ni kuwasaliti wakulima wa ndani.
“Soko lipo kubwa ila mazingira yake ndio hayajaandaliwa kwasababu bidhaa karibu  zote zinazotengenezwa na kampuni ya Azam, zinatumia unga wa mhogo yaani mikate,juisi na Bisukuti,viwanda vyote vya pombe wanategemea unga huo lakini unaweza kukuta wanaagiza kutoka nje”Anasema Wambura
Lakini faida ya Muhogo inaanza kwenye shamba kwani zao hilo linalovumilia ukame. Baadhi ya wadudu na magonjwa pia huhitaji kiasi kidogo cha rutuba. Muhogo ni zao la chakula na ni la nne kwa umuhimu katika nchi zinazoendelea za Bara la Afrika, Asia na Amerika ya Kusini. 
Kwa miaka mingi sasa muhogo  umekuwa ni zao linachukuliwa kama zao mbadala na zao la kimaskini barani Afrika. Ajabu ni kwamba inapotokea ukame na baa la njaa muhogo ndio mkombozi kwa watu wengi barani  Afrika.
Hivi sasa zao la muhogo limezidi kupata umaarufu zaidi, ambapo taratibi  kadri siku zinavyosogoea linabadilika   na kuwa zao la kibiashara. Katika  nchi nyingi za Afrika kama vile Afrika  ya kusini, Nigeria,Ghana, na kwingineko,  kuna viwanda vikubwa kwa ajili   ya kusindika mihogo.
Unga wa mhogo huzalisha  bidhaa  tofauti mojawapo ya bidhaa kubwa  zinazotengenezwa katika viwanda  hivyo ni pamoja na wanga kwa ajili ya  kutengenezea nguo, madawa, kiungo  cha kuongeza ladha kwenye vyakula,  pamoja na glucose inayotokana na  muhogo.
Mhogo unataajwa kuwa ni dhahabu nyeupe inayoweza kushindana na madini kutokana na soko lake kupanuka kuanzia shambani hadi sokoni huku zao hilo likitajwa kuwa halihitaji gharama kubwa kuwekeza.
 
“hapa nchini mhogo unahitaji kutengenezea pombe, kwenye viwanda vya bia,syrup ya madawa,gundi vindoge makampuni yanayotengeza juisi na biskuti wanaagiza nje kwa kuwa hapa ndani haaipatikani”anasema Wambura huku akisisitiza kuwa umefika wakati serikali itazame zao la mhogo.
Ofisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Kasam Maswaga anasema elimu ya kusindika muhogo ikienea katika maeneo mengi nchini miaka kumi ijayo zao la muhogo litakuwa ni zao kubwa na lenye heshima katika kuinua kipato cha mkulima kwa kulifanya kuwa zao la chakula na biashara.
“Sisi wataalam wa kilimo na serikali kwa ujumla tumelenga kuhakikisha zao la muhogo kupitia usindikaji linafikia kutumika kama zao la chakula na biashara kwa sababu hivi sasa tunaendelea kutoa mafunzo ya namna ya kulisindika hili zao na namna ya kulitumia”,anasema Maswaga.
 
Inatajwa kuwa Muhogo ni chakula kikuu cha karibu watu billioni moja katika nchi zaidi ya 105 duniani.  Zao hili huchangia zaidi ya theluthi moja ya mahitaji ya virutubisho vya kuongeza nguvu mwilini (calories); Utafiti umeonyesha kwamba zao la muhogo linaweza kusaidia nchi masikini kukabiliana na uhaba wa chakula na nishati. 
Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika. Karibu hektari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo.  Muhogo ni zao muhimu la chakula baada ya mahindi. Zao hili linachangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima. Inakadiriwa kuwa takribani kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini Tanzania.
Lakini Wambura anasema kuwa pamoja wingi wa uzalishaji huo bado takribani viwanda vyote haapaa nchini huagiza unga wa mhogo kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutegengenezea bidhaa zake huku wakulima wetu wakiachwa bila chochote.
Mikoa inayozalisha muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Tanga, Ruvuma, Mara, Kogoma, Pwani na Karibu maeneo yote ya Zanzibar. Ukanda wa Ziwa ni wazalishaji wakubwa zaidi ikifuatiwa na ukanda wa kusini. Mkoa wa Ruvuma huzalisha kati ya 5-10% ya uzalishaji wote Tanzania. 
Nchini Tanzania, muhogo unatajwa  kuwa zao la pili kwa kuchangia pato la taifa kwa asilimia 19 baada ya  mahindi. Pamoja na hayo, zao la muhogo lina faida nyingi sana ambazo humtoa mkulima katika wasiwasi wa kutumia fedha nyingi katika kununua dawa za mimea.
 Zao hili lina faida nyingi kijamii na hata kiuchumi na kwa maendeleo ya nchi. Ni zao ambalo linaweza kuzalisha bidhaa zaidi ya 300, zikiwemo zile za chakula na ambazo si za chakula viwandani. Unga wake hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali, baadhi ni uji na ugali, vitafunwa kama keki, mikate, biskuti, na maandazi. Majani yake hutumika kama mboga na dawa pia.
Katika viwanda, mazao yanayopatika katika mzizi wenyewe, miti na  majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu,  na plastiki. Vilevile wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali katika kuta za nyumba  na sukari(Sugar syrup).
 
 Kwa mara ya kwanza zao hili lililetwa na wareno, hapa Afrika. Zao hili hulimwa nchi zaidi ya 34 za Afrika kwenye eneo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari milioni 200.
 
 Kilimo cha mihogo huhitaji ujuzi  kidogo sana na ni rahisi kulima. Zao hili hustahimili ukame na huweza kubakia ardhini kwa muda mrefu kuepukana  na baa la njaa. Upatikanaji wa mavunoni wa uhakika kuliko mazao ya nafaka. Mizizi ya mihogo ndio tegemeo kubwa la wakulima. Mihogo huwa
na kiasi kikubwa sana cha VITAMINI ‘A’ na kiasi kidogo cha protini. Ulaji wa mihogo huwasaidia walaji kuepukana
na ugonjwa wa ukavu macho.
Pia majani ya mihogo huweza kutumika  kama mboga za majani maarufu kama  KISAMVU. Kuna kemikali iitwayo CYNOGENIC GLUCOSIDE ambayo  inaweza kuwa sumu kama mihogo   isipoandaliwa vizuri. Mihogo mitamu
ina kiasi kidogo sana cha kemikali hii   na huweza kuliwa hata Mibichi.
 
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimethibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe. Kiroba; Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
 

Maoni 4

Unknown alisema ...

Elimu nzuri sana hii. Je, ni wakulima wangapi wataona makala haya? Muda utaamua. Ubarikiwe na endelea kutupa elimu.

REMIGIUS WILLA alisema ...

Nashukuru kwa makala yako nzuri, lakini me nnashida moja ya kupata soko la muhogo au kiwanda chochote kinachochakata au kufanya any other kind of processing ya muhogo. kama unamjua mtu naomba anitafute kwwenye no 0672297498 tufanye biashara

Unknown alisema ...

Hekari moja bei gani

Bila jina alisema ...

Nahtaji kujua soko la kilimo nipo kigoma 0752527611