Wanasayansi watabiri kuwa Mwisho wa dunia huenda ukawa tarehe 26/8/ 2032.....Bofya hapa
Dunia tunayoishi, inaweza kufikia mwisho wake August 26,
2032. Kwa
mujibu wa wanajimu wa Ukraine, kimondo chenye upana wa futi
1,300
kinakuja kwa uelekeo wa duniani na kinaweza kuiponda dunia
kikiwa na
nguvu kubwa ya nuclear.
Crimean Astrophysical Observatory wamegundua kimondo kikubwa
kiitwacho
2013 TV135, weekend iliyopita na tayari jumuiya ya kimataifa
ya
wanasayansi imekielezea kama moja ya vimondo hatari kabisa
kuwahi
kugunduliwa angani.
Hata hivyo, bado, uwezekano wa kitu hicho kuiponda dunia ni
mdogo na
hivyo kuna asilimia 99.9984 za maisha kuendelea kama
kawaida. Kama
kimondo hicho kikiikosa dunia, kina uwezekano wa kupita
ndani ya maili
milioni 1 za mzingo (orbit) wa sayari hiyo.
Kama 2013 TV135 ikigongana na dunia kinakadiriwa kuzalisha
megatons
2,500 za mlipuko.
Hata hivyo kimondo hicho ni kidogo kuliko kitu kilichoiponda
dunia na
kuwaua wanyama wa zamani aina ya dinosaurs miaka milioni 65
iliyopita.
Kimondo hicho kilikuwa na upanda wa maili 6.
Kimondo hicho kitakuwa kimesogea zaidi mwaka 2024, na hivyo
kuwaruhusu
wanasayansi kuuchambua mzingo wake na wapi kitaangukia. Hadi
sasa,
kimondo cha 2007 VK184 ndicho kinaaminika kuwa na nafasi ya
kuiponda dunia.
Kimondo hicho chenye upana wa futi 420 kitakutana na dunia
mwaka 2048.
SOURCE DAIL MAIL.
No comments
Post a Comment