Taasisi za serikali jijini Daresalaam zimeanza kuleta tafrani kwa wananchi,Ni baada ya kutolea macho fedha za maegesho ya magari
Taasisi za serikali jijini Daresalaam zimeanza kuleta tafrani kwa wananchi baada ya kila taasisis kutaka kuendelea na kukusanya mapato ya maegesho katika jiji la Daresalaam,
Utafiti uliofanya na FUllhabari blog kwa kutumia wadau mbalimbali umebaini haya yafuatayo,
KWANZA KABISA MKURUGENZ I WA WAKALA WA UKUSANYAJI KODI ZA MAEGESHO (NPS) BW HASSAN KAHN AFUNGUKA
Mkurugenzi wa wakala wa ukusanyaji mapato ya magari ya maegesho, Bw. Hassani Khan ameelezea kusikitishwa kwake kwa tuhuma anazopewa na wanaofungiwa magari huko site na kusema kuwa watu hao wamekuwa hawamjui adu yao namba moja ni yupi na ni vipi wanaweza kwenda kupeleka malalamiko,yao.
Amesema wananchi hususani wale wanaofanyia shughuli zao hapa ilala wamekuwa wakiichukia kampuni ya NPS wakizani ndio wanaowafungia magari yao huko site wakati siyo kweli, na kubainisha kuwa ukweli ni kwamba wanaofunga magari hayo ni watu toka halmashauli ya Ilala ambao kwa hakika hawana weledi wa kufanya kazi ya kkusanya mapato hayo kwa wananchi,,
MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA NATIONAL PARKING SOLUTIONS BW HASSANI KAHN AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA MWANDISHI WA HABARI HIZI |
Amesema kutokana na muingiliano huo wa kimajukumu tayari kumekuwa na tatizo kubwa la kufanyakazi kwa ufanisi, kutokana na wananchi kutojua sasa ni nani wamlipe kati ya Halmashauli ya jiji na Halmashauri ya Ilala,
Tayari halmashauli ya Ilala imetoa zabuni ya ke na kuwakabidhi jukumu la kukusanya mapato kwa kampuni za Tambaza na Mwakibinga ambapo ama hakika wanawapa changamoto katika ufanyaji wa kazi zao za kila siku,
Muingiliano huo wa majukumu kwa taasisi za serikali kati ya halmashauli ya jiji na Halmashauri ya ilala tayari ni tatizo kwa mustakabali wa halmashauri ya jiji ambayo inafanya kazi ya kukusanya mapato hayo kupitia wakala huyo na kugawa mapato hayo kwa halmashauri zote za manispaa hapa Daresalaam,
MAPATO YAKOJE NA MMEJIPANGAJE KUHAKIKISHA KUWA MAEGESHO YA JIJI HAYAWI KERO,
Huyu hap mkurugenzi anafunguka,,Mkurugenzi wa kampuni hiyao ya kukusanya mapato ya maegesho anasema kwa sasa kampuni inafanya vizuri na tayari wamepatiwa mkataba mwingine na halmashauri ya jiji kuanza kukusanya mapato yake katika wilaya ya Temeke na Kinondoni ambapo hapo awali walikuwa hawafii,
Amesema kimsingi Halmashauri ya jiji imeona kunatija na kuendelea na sisi, kwania hatujawahi kuwaangusha katika target zao ambazo wamekuwa wakitupangia,,
amesema kwa mwezi tunatakiwa kukusanya si chini ya laki nane na kwamba ndani ya mwaka kampuni inapeleka katika halmashauri jumla ya TSH bil. 1 ambayo inatumika kwa manufaa ya wananchi,
AMESEMA PESA HIYO NI NETI AMBAYO HAINA MAKATO YEYOTE
Mkurugenzi Hassani Kahn amesema pesa ambayo inapelekwa ni sawa na asilimia themanini ya pesa inayokusanywa ambapo zingine ni kwa ajiri ya huduma ya uendeshaji wa ofisi,
kwa sasa NPS inajumla ya wafanyakazi ambao wanakusanya mapato wapatao 360 na wasimamizi 20 na staffs 18 ambapo jumla yake ina watu takribani 400 waloajiriwa katika kampuni hiyo,
WITO WAKE,
Ni kwamba ili kuondoa muingiliano wa kimajukumu kuna haja ya taasisi mbili hizi za serikali kuanza kukaa meza moja na kufuata ile sheria ya maegesho na 60 ya mwaka 1998.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni