SIKUMOJA TU BAADA YA WALIOBA KUMTAKA BULEMBO KUTAJA KAMA ANATUMWA NA CCM, NAPE AFUNGUKA, ATAJA MSIMAMO WA CCM
![]() |
KATIBU MWENEZI WA CCM, BW. NAPE NNAUYE AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WANAHABARI |
IKIWA NI SIKU MOJA TU TOKEA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI MSTAAFU JOSEPH WALIOBA KUSEMA HADHARANI KUWA MWENYEKITI WA WAZAZI CCM BW. BULEMBO KUWA TUME HIYO INAANDIKA MAONI YAO WENYEWE KATIKA MIKUTANOMBALIMBALI ALIYOIFANYA HIVI KARIBUNI, KATIBU MWENEZI WACHAMA HICHO TAIFA AMEIBUKA NA KUSEMA KUWA CHAMA CHAKE KINAMATUMAINI NA TUME HIYO NA KWAMBA WANAHESHIMU KAZI INAYOFANYWA NA TUME HIYO
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE, KATIBU HUYO WA UENEZI AMESEMA SISI KAMA CCM TUNA IMAANI NAKAZI INAYOFANYWA NA TUME, NA WANAIMANI NA JOSEPH WALIOBA NA KWAMBA WANAIMAANI KUWA WATAENDELEA KUA NA IMAANI NAO SIKU ZOTE
STORY YA BULEMBO MWENYEWE HII HAPA KAMA ULIKUWA HUJAIPATA
WARIOBA AMTOLEA 'UVIVU' BULEMBO
![]() |
Bw. Abdallah Bulembo |
NI KUHUSU TUHUMA ZAKE KWA TUME YA KATIBA
ADAI MAZINGIRA YA KAZI YAO NI MAGUMU SANA
Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imetoa ufafanuzi juu ya kauli mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa tume hiyo imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ngazi ya Wilaya iliyomalizika hivi karibuni
. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alisema siku zote tume hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa kujadili rasimu iliyotolewa badala ya kuhangaika na tume au wajumbe wake
Moja ya kazi za kisheria za tume ni kutoa elimu kwa umma ambayo ndiyo
kazi ya wakati wote," alisema Jaji Warioba wakati akijibu swali la
waandishi waliofika ofisini kwake kutaka ufafanuzi wa kauli ya
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw.
Abdallah Bulembo.
Bw. Bulembo amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akiwa mkoani Tanga na kudai kuwa, tume ya Jaji Warioba imeacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia uhuru wa wananchi wa kutoa maoni.
Jaji Warioba alisema, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao ndiyo wajumbe wa Mabaraza hayo, walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na wajumbe wa tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.
"Sasa (Bw. Bulembo) anaona kutoa elimu ni dhambi," alisema Jaji Warioba ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na kusisitiza kuwa, tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu.

No comments
Post a Comment