Zinazobamba

serikali kula kuku na mayai yake




SERIKALI Kuu na taasisi zake zimebainika kuwa chanzo cha kufirisika kwa
Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL),  kiasi cha kuwa taabani kifedha
kutoka tabia za taasisi nyeti za serikali zikiongoza kuwa wadaiwa sugu
wa madeni.Hatua hiyo inaifanya serikali ya Rais Kikwete kuwa sawa na
mfugaji wa Kuku anaye kula Kuku pamoja na mayai yake wakati bado ana
hamu ya kuendelea kufuga.


Akizungumza katika kikao kilichoukutanisha uongozi wa TTCL na Wizara ya
Mawasiliano, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundo Mbinu ya Bunge, Peter
Serukamba aliitaka Serikali kuziwezesha taasisi zinazodaiwa kulipa
madeni yao kufikia Desemba mwaka huu. Katika kikao hicho
kilichohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia, John Mngondo na Wajumbe wa Bodi ya TTCL, wakiongozwa na
Mwenyekiti, Edwina Lupembe na Ofisa Mtendaji Mkuu Kamugisha Kazaura.

Rais Kikwete akimlisha,Mkewe Mama Salma Kikwete,keki katika moja ya siku
za kuzaliwa kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam

“Kamati inapendekeza mkusanye madeni hadi Desemba tujue mmefikia wapi na
deni hili la bilioni 10. Ni fedha ambazo zingeweza kuwasaidia
kujiendeleza japo kwa kujikongoja, mbaya zaidi ni kwamba taasisi hizi za
Serikali hazioni umuhimu wa kuilipa TTCL kwa sababu nao ni mali ya
serikali,” alisema Serukamba. Alizitaja taasisi hizo na madeni yao
kwenye mabano kuwa ni Ofisi ya Rais (180.2 milioni) deni la miezi 21,
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( Sh 775.9 milioni) deni
la miezi sita, Jeshi la Polisi (773,154,278) deni la miezi 15, Jeshi la
Wananchi la Tanzania (2.1 bilioni) ikiwa ni gharama ya huduma mbalimbali
zinazotolewa na kampuni hiyo.

Taasisi nyingine ni Jeshi la Polisi (Sh1.28 bilioni) miezi 32 kwa huduma
za takwimu na simu, wakati Sh360 milioni kwa huduma za kukodisha vifaa,
wakati Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) inadaiwa Sh50
milioni baada ya kupata huduma kwa miaka sita. Kamati hiyo pia imeitaka
Serikali ifanye mchakato wa kuitoa TTCL kwenye ubia na Airtel ili
kuidhamini kwenye taasisi za kifedha ili iweze kukopesheka .

No comments