MTEMVU AMWAGIWA SIFA KWA KUWA KINARA WA MAENDELEO TEMEKE
Mbunge
wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (kushoto), akihutubia na kummwagia sifa
Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa wabunge wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia), kwa tabia yake ya kuwa karibu na
jamii na kutetea maendeleo ya Temeke na Dar es Salaam jana katika
mkutano wa jimbo hilo wa kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa
jimboni (HD)
Mbunge wa
Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akihutubia katika mkutano wa
jimbo uliofanyika eneo la Lumo, Kata ya Yombo Vituka, Dar es Salaam,
ambapo pamoja na mambo mengine alielezea miradi mbalimbali ya maendeleo
iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.
Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa akihutubia katika mkutano wa
Jimbo la Temeke eneo la Lumo, Yombo Vituka, Dar es Salaam , ambapo
pamoja na mambo mengine aliwataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
na Serikali kuwajali vijana kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali
zinazowakabili. Kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtemvu,
Meya wa Ilala, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
No comments
Post a Comment