NCCR MAGEUZI YATOA SOMO KWA WANASIASA WA TANZANIA,YAPOKEA WANACHAMA WAPYA
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama, Ndg. Mosena Nyambabe akiongea na waaandishi
|
CHAMA cha NCCR mageuzi kimesema Siasa za Tanzania zimepoteza mwelekeo,kutokana
na kuwepo kwa wanasiasa wasio kuwa na uchungu wa nchi.
Hayo yameibuliwa leo na Kaimu katibu mkuu wa chama NCCR Mageuzi Ndg
Mosena Nyambabe, wakati akizungumza na waandishi wa Habari ,Ofisi za Makao
makuu ya NCCR.
Nyambabe amesema kwa sasa siasa za Tanzania zimepoteza mwelekeo kutokana
na kuwepo kwa wanasiasa wasiokuwa na uchungu wanchi yetu.
“kwa hali ya siasa zetu za Tanzania kama ni mfwatiliaja wa siasa utajua kuwa
siasa zetu zimepoteza mwelekeo kwa kutokana na wanasiasa wasiokuwa na
uchungu wan chi yetu”
Nyambabe ametoa sababu za siasa zetu kupoteza mwelekeo na kusema imetokana na
chuo kikuu cha Dar es salaam kuacha kutoa agenda na mwelekeo kwa serikali
“kabla ya mwaka 1990 Chuo kikuu cha dar es salaam kilikuwa kinaandaa
makongamano ya kutoa agenda kwa wanasiasa pamoja nakuishahuri Serikali”
“ lakini katika hali ya kushangaza baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama
vingi chuo kikuu cha mlimani kimeacha kufanya hivyo matokeo yake wamewaachia
wanasiasa matokeo yake ni kupoteza mwelekeo”alisema Nyambabe
Vilevile katika hatua nyingine chama cha NCCR mageuzi kimewapokea
wanachama wapya ambao wamehamia chama hicho kutoka vyama vingine vya siasa
nchini.
Wanachama hao ni pamoja na Ramadhani Manyoko ambaye alitokea PPT
maendereo ambapo alikuwa Naibu katibu mkuu mkoa wa Tanga pamoja na Lilian
kitunga aliyetokea Chama cha Demokrasia CHADEMA ambapo yeye ni mwananchi wa
kawaida
Wote kwa pamoja walisema wamejiunga na NCCR mageuzi kutokana na cham hicho kuwa
na Dhamila ya dhati ya kumuinua mtanzania kwa kuweka nchi kwanza mengine
yanafwata.
Na
karoli Vinsent
Hakuna maoni
Chapisha Maoni