DANGULO LINALODAIWA KUTMIKA NA MADENTI WA VYUO VIKUU LAFUMULIWA
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na Global Publishers wamefanikiwa
kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo mbalimbali jijini
Dar.
Madenti hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro
hilolililopo ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya
Buguruni-Sokoni, Dar.
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa
eneo hilo, waandishi hao
waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana
kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya waandishi hao
walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za kutosha huku wakiwarekodi wahusika
(madenti wanaojiuza na wanaume wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya
kazi bila wao kushtuka.
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia buku mbili hadi tano na
wa bei
mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na
kuendelea.
Mmoja wa waandishi hao
alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji ambapo alipofika na kujionea
mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo kuwa alikuwa amepokea simu ya
dharura.
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani, anasimulia:
“Nilishuhudia watu
wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom
ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani
nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali
ile tumekwisha.”
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua danguro hilo, waandishi
hao
waliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo.
Bila kusita, kamanda huyo aliteua vijana wake kutoka Kituo
Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika
wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.
*DENTI IFM*
Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa na polisi, mmoja wa
madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake
aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.
Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi
hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja hicho cha maasi ni
denti
aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo)
ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa
akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.
Denti mwingine aliyekamatwa katika msala huo alijitambulisha
kwa jinamoja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja
kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni
wanafunzi.
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa njemba mmoja aliyekuwa
ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza kondom kwa madenti hao
ambao humwingizia kipato chapuchapu.
Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako
maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao walikamatwa huku
mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza
mwili.
*YUMA YA NONDO*
Baada ya kuhojiwa kuhusika na biashara haramu ya ngono na
kukiri,watuhumiwa hao wote waliwekwa nyuma ya nondo kwenye Kituo
cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la kesi namba
BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni