VITUO VYA DALADALA VYA UBUNGO NA MWENGE KUHAMISHWA>>>>>> SOMA HAPA UJUE VINAPELEKWA WAPI,
VITUO vya daladala vya Ubungo na Mwenge vinahamishwa kupisha
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart), ambao
miundombinu yake
inaendelea kujengwa.
Kituo cha Ubungo kitahamishiwa nyuma ya jengo la Mawasiliano
lililopo Barabara ya Sam Nujoma, vivyo hivyo kituo cha Mwenge,
kitatumika kwa ajili ya kushusha abiria pekee.
Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera
amesema, magari ya Mwenge, yatakuwa na uamuzi wa ama kuishia kwenye stendi
ya Makumbusho ;au kwenda hadi kituo hicho kitakachohudumia magari ya
Ubungo kilichoko
Mawasiliano.
Kwa mujibu wa Mhowera, wakati wowote kuanzia sasa vituo
hivyo, vitabomolewa kupisha mradi huo.
Hata hivyo, hakuelezea kwa undani juu ya maandalizi ya
ujenzi wa kituo hicho kipya. Alisema hayo alipozungumza na mwandishi wa
habari hizi,kuhusu hatua zinazochukuliwa na manispaa, kuwezesha
wafanyabiashara ndogo kupata maeneo ya kuendesha shughuli zao.
Alisema baada ya kituo cha Ubungo kuhamishiwa katika eneo
hilo jipya,hakutakuwa na mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza bidhaa
zozote kama ilivyo sasa.
Alisema kuhamishwa kwa vituo hivyo, kutatoa nafasi kwa
wafanyabiashara kwenda katika maeneo waliyopangiwa kwa kuwa hakutakuwa na
nafasi, kwani yote yatatumika kwa ajili ya barabara.
“ Kwa hiyo ni bora wakaanza kujiondosha wenyewe mapema kabla
hatua ya kuondolewa na ujenzi kuwafikia,” alisema.
Kwa mujibu wa ofisa habari huyo, yapo maeneo yaliyotengwa
kwa ajili yakazi hiyo katika masoko mbalimbali likiwemo laKijitonyama.
-Habari leo
No comments
Post a Comment