MTUHUMIWA SUGU AKAMATWA MKOANI SIMIYU,....>> SILAHA 45 ZA KIVITA , 17 ZA KIENYEJI NA SHEHENA ZA RISASASI ZAKAMATWA
OPERESHENI Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu
kukabiliana na vitendo vya Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na
wahamiaji haramu umefanikisha kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za
Kivita na 17 za kienyeji na risasi 892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu
wa ujambazi na ujangiri wakitiwa mbaroni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi.
Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini
kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi alisema kuwa
opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya
tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya
Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.
Silaha zilizokamatwa za kisasa na za kienyeji.
Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na
magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa
na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa
Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13
zilisalimishwa kwa hiali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.
Shehena ya risasi zilizo kamatwa.
“Tumeweza pia kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya
uhalifu ambaye
hivi karibuni aliachiwa kutoka Gerezani lakini tukapata
taarifa za raia wema kuwa amekuwa akijihusisha na ujangiri na ujambazi
ambaye ni Masanja Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na SMG
moja na risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa pia na silaha”
alisema.
Silaha za zilizotengenezwa kienyeji.
Kufatia operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa
kuwakamata wahamiaji haramu wane katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya
watu kumi waliokuwa wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za
serikali ikiwa ni za wanyama waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
na Mapori ya Akiba katika Wilaya za Meatu, Maswa na Itilima.
“Tumeunda kikosi kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni
ya
kuwakamata wafugaji na mifugo yao ambao wamekuwa wakichungia
mifugo ndani ya eneo la Hifadhi ya Serengeti ambapo zaidi ya
ng’ombe wengi
walikamatwa na kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi
milioni 180
zilipatikana huku watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri
wakiuwa tembo na wamyama na kuuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani”
alisema Kamanda.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la
Polisi kutoa taarifa za siri zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na
wahamiaji haramu katika maeneo yote ya Wilaya za Meatu, Maswa,
Bariadi, Itilima na Busega huku makakati wa kuanzisha vikosi kazi kila tarafa
ukiwa mbioni kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.
source: GSENGO
Hakuna maoni
Chapisha Maoni