Zinazobamba

MATOKEO DARASA LA SABA HAYA HAPA, WANAFUNZI LAKI NNE WAFAULU KATI YA LAKI NANE,

BALAZA LA MITIHANI TANZANIA NECTA LIMETANGAZA MATOKEO YA DALASA LA SABA KWA MWAKA 2013/2013 AMBAPO JUMLA YA WANAFUNZI LAKI NNE WAMEFANIKIWA KUFAULU MTIHANI HUO 
NATANGAZA>>>> KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BALAZA LA MITIHANI TANZANIA DKT. CHARLES MSONDE AKITANGAZA MATOKEO YA DALASA LA SABA MAPEMA HII LEO,

Mtihani huo ambao ulifanywa na jumla ya wanafunzi 844,983 umeshuhudiwa wanafunzi jumla ya 427,606 wakipata alama zaidi ya 100 katika alama 250 ya masomo yote, kwa maana ndo waliofaulu huku nusu yake wakitoka patupu, 

Katika mchanganuo wa ufaulu huo, wasichana walikuwa 208,227 ambao ni sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 ambao ni sawa na asilimia 55.01, miongoni mwao pia wamo wenye ulemavu 476 (ambapo wasichana ni 219  sawa na asilimia 46.01 na wavulan ni 257 sawa na asilimia 53.99 ya watanzania wote wenye ulemavu waliofanya mtihani)

UFAULU KIMASOMO (kiswahili lapeta, hisabati bado kigugumizi kwa wanetu)
Takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa somo la kiswahili wanafunzi wamefaulu sana huku somo la Hisabati likiendelea kuwa tatizo kwa wanafunzi wetu, somo la kiswahili wanafunzi wamefaulu kwa wastani wa asilimia 69.06 huku somo la hisabati likiwa 28.62

MATUMIZI YA OPTICAL MARK READER (OMR) YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

Matumizi ya opticala mark reader imeonesha mafanikio makubwa wa kusahihisha mitihani hiyo kwa usahihi zaidi ukilinganishwa na ile iliyosahihishwa kwa mkono

Akizungumza na wanahabari katika ofis hizo , Dkt Msond amesema ili kujiridhisha walitenga baadhi ya wanafunzi zaidi ya mia mbili toka wilaya 48 za mikoa 9 na kubaini kuwa karatasi zilizosahihishwa kwa mikono zinamakosa makubwa.

Amesema makosa hao ni aidha waweke pata pale ambapo kuna kosa ama waweke kosa pale ambapo kuna pata  kitu ambacho katika karatasi zilizosahihishwa na compyuta hakuna kitu hicho,
Kaimu mtendaji wa balaza akionyesha baadhi ya karatasi maalum zilizotumika katika kusahihisha mitihani ya dalasa la saba


AIDHA katka matokeo hayo pia jumla ya wanafunzi 13 wamefutiwa matokeo yao kutokana na sababu mbalimbali, zingine zikiwa ni kurudia dalasa pasipo ruhusa ya balaza huku wengine wakikamatwa na vikaratasi katika chumba cha mtihani

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,kaimu katibu mtendaji wa balaza la mitihani Tanzania, Dkt.Charles Msonde amesema kuwa ufaulu wa masomo katika mwaka huu uepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ikilinganishwa na mwaka jana
Matokeo ya dalasa la saba pia yanapatikana katika tovuti ya    
  • www.matokeo.necta.go.tz,
  • www.necta.go.tz au www.moe.go.tz na
  • www.udsm.edu.ac.tz

Hakuna maoni