Zinazobamba

MCHAKATO WA KATIBA MPYA NI MWIBA, VYAMA VYA SIASA VYASEMA TUKO NJIA PANDA , KIBAMBA AWAITA KATIKA MASHAURIANO


MCHAKATO WA KATIBA UMEENDELEA KUWA KITENDAWILI KUFUATIA WADAU MBALIMBALI KUONYESHA DALILI ZA KUTOKUWA NA IMAANI JINSI MCHAKATO MZIMA UNAVYOENDESHA NA WENGINE KUSEMA KUWA UMEHODHIWA NA CHAMA KIMOJA

MWENYEKITI WA JUKATA BW. DEUSI KIBAMBA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA VYAMA VYA SIASA VILIVYOHUDHULIA KATIKA KIKAO CHA MASHAURIANO,KWA PAMOJA WAMESEMA KUWA KUNA HAJA YA RAISI ASISAINI RASIMU YA KATIBA NA KUSUBILI KWANZA VIPENGELE VINAVYODAIWA KUREKEBISHWA IKIWEMO IDADI YA WASHIRIKI KATIKA BUNGE LA KATIBA NA NAMNA LITAKAVYOENDESHWA
WAKIZUNGUMZA KATIKA MEZA YAMASHAURIANO ILIYOITISHA NA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA, MWENYEKITI WA JUKWAA HILO BW. DEUSI KIBAMBA AMESEMA BADO SUALA HILI LIMEKUWA NJIAPANDA KUFUATIA WATU MBALIMBALI KUWA NA MALENGO YASIYO FANANA

AMESEMA SUALA LA KUTUKA KATIBA MPYA NI LAZIMA LIWE SHIRIKISHI NA KWAMBA KINYUME CHOCHOTE KILE JUKWAA WAMEJIPANGA KUHAKIISHA KUWA WANANCHI WANAPIGA KURA YA HAPANA KUHUSIANANA KATIBA HIYO,
RAIS MTENDAJI WA IPPT MAENDELEO BW. PETER KUGA MZIRAY AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO WAMASHAURIANO,MZIRAY AMESEMA HAKUNA MANTIKI YA VYAMA KWENDA KUKUTANA NA RAIS KWANI MAMBO YA MSINGI YOTE YAYODAIWA AMEYASIKIA NA KINACHOSUBIRIWA NI MAJIBU YAKE TU,KWA MUJIBU WAKE NI KWAMBA KUITA VYAMA VYA SIASA VITATU VIKAKUTANE NAE NI KUONYESHA KUWA MAKUNDI MENGINE YA KIJAMII HAYANA UMUHIMU.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA NLD DK. EMMANUEL MAKAIDI AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WADAU WA VYAMA VYA SIASA VILIVYOKUTANA JIJINI DARESALAAM

MBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI BW. JOHN MNYIKA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WADAU HAO, MNYIKA AMESEMA KUWA HAONI SABABU YA KWENDA IKULU KWANI TAYARI WALISHAKUTANA NA MUHESHIIWA RAIS,

TUNAFUATILIAAA, VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKIFUATILIA MKUTANO HUO MAPEMA HII LEO JIJINI DARESALAAM

No comments