Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini
Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza
mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na
kupokelewa na wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa
biashara.

Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo
siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25
iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo,
Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari
kama Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station,
Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.
Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa alipata
kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo
ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha
ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari
kushirikiana na Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa miundombinu
ikiwemo bandari, ujenzi wa madaraja na bandari. Dr. Slaa na mkewe
Josephine walipokelewa na Gavana pamoja na mawaziri wake

Dr. Slaa akiwasili kwenye gavernor mansion baada ya kupokelewa na Waziri wa Biashara pamoja na Waziri wa mambo ya nje

Viongozi wa juu wakibadilishana mawazo na Dr. Slaa

Dr. Slaa Akimkabidhi Waziri wa Biashara Sera za Kiuchumi za Chadema

Dr. Slaa, gavana na mawaziri wake wakiwa katika mjadala wa ushirikiano

Dr. Slaa kwenye picha ya pamoja na gavana

Gavana akimnong'onezea Dr. Slaa neno wakati wa kuagana

Dr. Slaa akiongozwa kuelekea kwenye msafara wake

Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake
Dr. Slaa akimshukuru mmoa wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake
Kubwa ya yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza kuwa na
ufanisi hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita
tu, huku CCM ikiwapa walipa kodi wa tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na
kazi. Wengi wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua
sakafuni, walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali
duni na wanafunzi wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa
lililowakumba watanzania
Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn
Kadhalika Dr. Slaa ametembelea chuo kikuu cha auburn ambayo ni moja ya
vyu vikuu vikubwa zaidi vya utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli
zake nchini Kenya, Uganda, Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini
Kenya, chuo cha auburn inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa
samaki na technologia za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi
kwenda ulaya Ulaya. Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya
ajira 7000.
Walipoulizwa kwa nini walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena
kwamba ni vigumu sana kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa
wangekuja na fedha zao kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la
USAID ambayo inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo
Kenya na Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania
ikiwa mazingira ya kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala,
ambayo Mh. Slaa amewahakikishia kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao
kazi.
Viongozi wa Auburn University wako tayari kusaidia vyuo vya Tanzania
kama Sokoine kwa kuwafundisha waalimu na pia kubadilishana nao
technolojia za kisasa za kilimo. Wako pia tayari kuwafundisha wakulima
wa aina zote na hata walaji mbali mbali mbali.

Dr. Slaa akiwasili chuo kikuu cha Kilimo Cha Auburn. Nyuma yake ni walinzi kwenye msafara wake

Dr. Slaa akilakiwa na Dean wa Chuo cha Kilimo pamoja na viongozi wengine wa juu wa chuo hicho

Dr. Slaa akiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa chuo cha kilimo
kushirikiana na vyuo vikuu vya tanzania kwa lengo la kubadilishana
teknolojia na ujuzi ili kuinyanyua kilimo cha tanzania na pia kuongeza
ajira
No comments
Post a Comment