VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA SASA YAPAMBA MOTO, MWINGINE AKUTWA AMEKUFA NA MADAWA YAKE TUMBONI,
Jeshi la polisi linawashikilia watu wawiwili wanaofahamika kwa jina laa Nasri Omari MAARUFU Roboti na Mwanaisha kapama ambao wamekutwa na mtu mmoja alifahamika kwa jina la Rajabu kidunda akiwa amekufa ghafla huko maeneo ya Tabata,
Kidunda ambae aliingia katika jiji la daresalaam mapema wiki iliyopita alikutwa amekufa katika chumba cha bw. Nasri Omari wakati akitoka bafuni kuoga
jeshi hilo limesema baada ya kuuchunguza mwili huo wamefanikiwa kuuona ukiwa na pipi za madawa ya kulevya 33 aina ya Heroine yenye thamani ya mamilioni,
Aidha katika upekuzi huo pia walimkumta na fedha mbalimbali za nchi jirani ikiwemo nchi ya kenya shelisheli na dolla 100
HAYA NDIYO MADAWA AMBAYO MAREHEMU ALIUKUTWA NAYO TUMBONI |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kamishna wa polisi kanda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA amewataja watuhumiwa hao kuwa ni NASRI OMARI na MWANAISHA SALIMU wakazi wa kigogo luhanga.
Madawa hayo yalikamatwa maeneo ya tabata ambapo KOVA amesema kua polisi walpata taaifa kuwa kuna mtu mmoja amefariki hghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni kuoga ndipo walipofika nyumbani kwa NASRI OMARI na kuhoji hatimae kugundua uwepo wa maiti sebuleni iliyouwa imelazwa chali.
Kwa mujibu wa mmliki wa nyumba hiyo NASRI alisema kuwa marehemu anajulikana kwa jina la RAJABU KIDUNDA .
Polisi wamesema kuwa marehemu alifika toka mtwara na alipokelewa na watuhumiwa hao wawili ,ambapo wate wanashikilia kwa uchunguzi zaidi
KAMISHNA KOVA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA LEO |
BAADHI YA WANAHABRI WAKISIKILIZA KWA MAKINI |
No comments
Post a Comment