BIDHAA ZA VYAKULA ZAPUNGUZA MFUMUKO WA BEI
Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Agosti, 2013 umepungua hadi
kufikia asilimia 6.7 kutoka asilimia 7.5 za mwezi Julai, 2013 kutokana
na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Agosti 2013 leo Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema
kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kumechangiwa na kupungua kwa bei za
bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kutoka asilimia 8.0 kwa mwezi
Julai, 2013 hadi asilimia 6.5 za mwezi Agosti, 2013.
Kwesigabo amefafanua kuwa kasi ya ongezeko la bei kwa bidhaa zisizo za vyakula imebaki kuwa asilimia 7.3 kwa mwezi Agosti, 2013 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2013.
Kwesigabo amefafanua kuwa kasi ya ongezeko la bei kwa bidhaa zisizo za vyakula imebaki kuwa asilimia 7.3 kwa mwezi Agosti, 2013 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2013.
“Kupungua kwa Mfumuko wa Bei kunamaanisha kuwa, kuna unafuu wa maisha kwa mlaji; kwa maana hiyo Tanzania inaonyesha kuwa inapiga hatua nzuri katika uchumi wa nchi yetu”, amesema Kwesigabo.
Amezitaja bidhaa za vyakula
zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kuwa ni pamoja na mikate na
nafaka (asilimia 2.2), vitafunwa (asilimia 3.8), mahindi (asilimia 1.6),
unga wa ngano (asilimia 2.5), unga wa muhogo (asilimia 0.6), mtama
(asilimia 3.4) na kuku wa kienyeji (asilimia 0.9).
Bidhaa nyingine ni samaki wabichi
(asilimia 2.6), karanga (asilimia 2.0), mbogamboga (asilimia 2.4),
nyanya (asilimia 9.9), vitunguu maji (asilimia 2.0), viazi vitamu
(asilimia 4.8), mihogo (asilimia 4.1) na sukari (asilimia 0.5).
Bidhaa zisizo za chakula zilizochangia
kupungua kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na; viatu (asilimia 0.3), samani
(asilimia 0.1), vyombo vya udongo (asilimia 1.0), na vifaa vya
elekroniki vya kurekodia picha na sauti (asilimia 0.3).
Wakati huohuo Mkurugenzi Kwesigabo
amesema kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi agosti, 2013
imepanda ikilinganishwa na mwezi septemba 2010.
Akitolea mfano wa shilingi 100,
Kwesigabo amefafanua kuwa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma umepungua hadi kufikia Shilingi 71 na Senti 46
kwa mwezi Agosti 2013.
“Hii inamaanisha kuwa, ili Mlaji aweze
kununua bidhaa na huduma sawa na alizokuwa akinunua kwa Shillingi 100
mwezi Septemba, 2010 atahitaji Shilingi 28 na Senti 54 zaidi, yaani awe
na Shilingi 128 na Senti 54 mwezi Agosti, 2013”, amesema Kwesigabo.
Mfumuko wa Bei nchini umeanza kuonyesha mwelekeo unaofanana na nchi jirani za Afrika mashariki hususani Kenya na Uganda.
No comments
Post a Comment