SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA JN-NYERERE,RUNGU LAWASHUKIA WALIOSAIDIA KUSAFIRISHA MADAWA YA MASOGANGE
Sakata la kusafirisha madawa ya kulevya kwenda Afrika kusini
limechukua sula mpya baada ya waziri mwenye dhamana ya uchukuzi hapa nchini Mh.
Harison Mwakiyembe kuchukua hatua kali dhidi yao ikiwamo kuwafukuza kazi
mtandao mzima ulihusika kuasaidia kwa namna moja ama nyingine upitishwaji wa
madawa hayo,
Akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwa waziri
Mwakyembe amebainisha baadhi ya ushahidi ulitumika kugundua mtandao mzima
uliohusika kusaidia kusafirisha mzigo huo wa madawa ya kulevya katika uwanja wa
ndege wa mwalim Jurius kuwa ni kamera zilizofungwa katika uwanja huo
| Waziri wa uchukuzi akionyesha picha ya msanii agness gelard maarufu kwa jina la masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko afrika kusini. |
| waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini waziri wa
uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na serikali kuushugulikia
mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya
|
Akiwataja watu ambao wamehusika kusafirisha mzigo huo,ni
pamoja na askari wa polisi CPl Ernest
alionekana akiwa bize na kuoneka na kila dalili ya kusaidia kusafirisha mzigo
wa aina yake siku hiyo
Wengine ni walinzi wa uwanja huo ambao Yusuph Isa,Jackson
Manyoni,Juliana Thadei Na Mohamedi
Kalungwana ambao wote kwa pamoja walisaidia
kusafirisha madawa hayo na hivyo wizara kuiamuru muajiri wa wafanyakazi hao
kuwafukuza kazi mara moja na wasikanyage uwanja wa ndege
Pia askari ambaye amehusika na kula nyama za kusafirisha
madawa hayo wizara wameitaka jeshi la polisi kumshughulikia askari huyo
ipasavyo na kwamba wizara inatarajia askari huyo hawezi kukanyaga tena uwanja
wa ndege
No comments
Post a Comment