MKUTANO WA WAZIRI KAWABWA WAINGIA DOA, KUNDI LA WANANCHI LAVAMIA NA KUSHUSHA VILIO KAMA WATOTO WADOGO, WADAI FIDIA ZAO
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu
lililojitambulisha kuwa ni waathirika wa mpango wa ujenzi wa chuo cha afya cha
muhimbili (MUHANS) huko Kibamba –Mlonganzilo lilizusha sekeseke kwenye mkutano huo
baada ya kushusha vilio mfululizo mbele ya umati mkubwa ulihudhulia uzinduzi wa
matokeo makubwa sasa
Kundi hilo lililofika mapema majira ya asubuhi lilianza
sakata hilo majira ya saa nane ambapo walianza kulia kwa sauti kubwa huku
wakijilaza chini wakitaka magari ya viongozi wa wizara ya elimu yasiondoke ili
wapatiwe ufumbuzi wa tatito lao lilowaleta katika mkutano huo
Taharuki hiyo ilikuja kufuatiwa kundi hilo kuambiwa
uwezekano wa kuonana na waziri haupo kwani tayari ameshaondoka katika eneo la
tukio, hivyo ni bora waondoke watafute siku nyingine ya kuonana naye maneno
yaliyotafsiliwa na kundi hilo kuwa ni dhalau ya hali ya juu iliyoonyeshwa na
waziri kwa kundi hilo
Akizun gumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa waathirika
waliofanya taharuki ya aina yake katika mkutano huo Bi.Maria Daudi amesema
tatizo lao kubwa hadi kufikia hatua ya kulia hadharani ni kutokana na hatua
inayofanywa na wizara ya elimu ya kushindwa kulipwa fidia zao kwa wakati huku
wao wakiwa hawana sehemu ya kuishi hali inayowafanya waishi kama wakimbizi
katika taifa lao
“Waziri ameamua kutukimbia wakati anajua wazi kuwa tumekuja
hapa ili atutatuliye kero zetu lakini yeye anaamua kutokea mlango wa nyuma hivi
kweli tunajenga taifa la namana gani kama waziri mwenye dahamana unaogopa
wananchi wako kuwapa ukweli”aliongeza
Bi. Daudi ameendelea kusema kuwa mwezi wa saba mwaka jana walilazimishwa
kuvunjiwa nyumba zao bila kupewa taarifa mapema hatua iliyowafanya kwenda kwa
mkuu wa mkoa ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lao lakini mpaka hii leo bado
hawajapatiwa maelezo ya kueleweka zaidi ya kuzungushwa kila kukicha
“Ndu mwandishi sisi kama unavyotuoa hapa toka asubuhi tupo
hapa,kwanza tuliambiwa twende wizarani tulipofika wizarani tukaambiwa waziri
hayupo ameenda katika mkutano huko viwanja vya gymkana na ndipo tukaamua kuja
kumuona lakini mpaka sasa hatumuoni huyo waziri”aliongeza kusema Bi Daudi
Mwandishi wa habari hizi alipotaka kujua kulikoni waziri
ametoweka ghafla na kushindwa kuwaona wananchi hao ambao walikuwa na shauku
kubwa ya kumuona,afisa habari wa wizara hiyo Bw. Ntambi Bunyazy amesema kwa
wakati huo waziri tayari ameshaondoka katika eneo la tukio na hivyo ingekuwa
vigumu
kuweza kuonana naye
Aidha akizungumzia sakata hilo afisa huyo wa habari amesema,
suala la wananchi hao linafahamika, ila kwa sasa kuna mtu amejitokeza na
kufungua kesi mahakamani akidai kuwa kundi hilo linalodai fidia sio halali na
kwamba anayestahili kulipwa fidia ni yeye kwani ndio mmiliki halali wa eneo
hilo
Kwa sasa suala hilo liko mahakamani hivyo nisengependa
kusema lolote, tusubiri tuone na kama wao wanahaki ya kulipwa basi stahiki zao
zitalipwa baada ya kuamuriwa na mahakama,aliongeza Bw.Bunyazy
CAPTION
001)MMOJA wa wananchi hao
wakionyesha moja ya nakala walizokabidhiwa ili kupatiwa malipo yao
2)MARIA DAUDI akijilaza chini huku
akisaidiwa na msamaria mwema katika ukumbi huo wa mwalimu Nyerere, maria
alijigaragaza chini huku akitaka waziri atoke ili kumueleza shida yao,Bi. Daudi ni mama mjane na tegemezi lake ni nyumba
ambayo tayari amevunjiwa
3)MMOJA wa kundi hilo akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari
mwisho
No comments
Post a Comment