RESTLESS NA TEYODEN KUKUTANISHA VIJANA KUHUSU RASIMU YA KATIBA
Shirika la RESTLESS kwa kushirikiana na mtandao wa vijana manispaa ya Temeke
(TEYODEN) watawakutanisha vijana katika vikundi mbalimbali vya manispaa ya Temeke
ili kujadiliana kwa pamoja juu ya mapendekezo ya vijana katika rasimu mpya ya
katiba katika mradi uliopewa jina “KIJANA WAJIBIKA”
Wakizungumza katika kikao cha makubaliano ya ushirikiano huo
msimamizi wa mradi huo kwa mkoa wa Dar
es salaam kutoka RESTLESS Ridhiwani Juma
alisema kuwa wameamua kushirikiana na TEYODEN katika mradi huo kwa kuwa ndiyo
mtandao pekee wa vijana manispaa ya Temeke uliotapakaa kata zote za manispaa
hiyo.
Mradi huo wa kijana wajibika utatoa fursa kwa vijana wa
manispaa ya Temeke kuweza kukaa katika vikundi vyao na kujadilana kwa pamoja
juu ya elimu ya kujitambua na uelewa wa kijana katika mchakato wa kupata katiba
mpya.
“Vijana wataangalia kwa upana wake rasimu ya katiba mpya
kuhusu mambo ya elimu ,afya,ajira,stadi za utetezi ushiriki na ushirikishaji na
mambo muhimu ya kupata uongozi kwa vijana yalivyozungumzwa katika rasimu ya
katiba mpya” alisema Ridhiwani
Aidha ridhiwani alisema kuwa mradi huo ambao unafanyika
katika wilaya zote za jijini Dar es salaam na mikoani utakuwa ni wa kipindi cha
miezi 18 kuanzia mwezi nane mwaka huu hadi january 2014 na watatengeneza mtandao wa vijana wanaojua
kusoma na kuandika na wanaoweza kujieleza vizuri na wakaeleweka kwa jamii.
Ameongeza pia watatumia vipindi vya redio kwa kuwatumia
vijana wanaoweza kujieleza vizuri na
mawazo yao yakasikilizwa kitaifa na kila wilaya watachagua kijana mmoja ambaye
atahudhuria mafunzo ya siku tatu katika mkoa wa morogoro ambayo yanataranjiwa
kuanza muda wa wiki moja ijayo gharama zote zitakuwa za RESTLESS
Vilevile Ridhiwani aliongeza kuwa kwa vikundi katika wilaya
vitakuwa vinakutana kwa siku nne ambazo wao RESTLESS watagharamia vinywaji na
nauli kidogo kama mpango huo utaenda sawa na bajeti waliopanga.
Kwa upande wake katibu wa TEYODEN Yusuph Kutegwa alisema
kuwa mpango huo ni mzuri wa vijana wa Temeke kwa kuwa hakukuwa na kitu kama
hicho cha kuhakikisha mawazo ya vijana wa Temeke yanaingizwa katika mchakato wa
katiba mpya
No comments
Post a Comment