ISSUE YA PONDA BADO PASUA KICHA, KOVA AWATUPIA MPIRA MADAKTARI ADAI WAO WATASEMA KAMA KAPIGWA RISASI AU LAA, BAKWATA NAO WATOA NENO
BARAZA
kuu la waislam Bakwata limelaani kitendo cha kupigwa na kuumizwa kwa kitu
kisichojulikana kwa katitibu wa Jumuiya na Taasisis za Kiislam Sheikh Issa
Ponda na kumtaka Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Phaustine Shilogile kujiuzuru.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es
salaam Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum amesema kuwa BAKWATA
imesikitishwa na kitendo hicho kwani ni kinyume cha haki za Binadamu hivyo ni
vema tume huru ikaundwa wakati Kamanda Shilogile akiwa amejiuzuru ili kupisha
uchunguzi huru kufanyika ili kujua kama Jeshi la Polisi ndilo lililohusika na tukio
hilo la kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.
Alhad amesema kuwa hadi sasa BAKWATA haijapata
taarifa rasmi kutoka kwa Daktari na Jeshi la Polisi kama amejeruhiwa na risasi na kulitaka jeshi
la polisi kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa tukio hilo kuchukuliwa hatua madhubuti
za kisheria pindi watakapobainika kuhusika.
12-AUG-BAKWATA.
Aidha Sheikh Alhadi amesema kuwa pamoja na
kutofautia kifikra na kirai bado Sheikh Ponda ni kiongozi mwenzao na BAKWATA
haina uadui na sheikh Ponda na ndiyo maana wameamua kutoa masikitiko yao kwa
kitendo cha kinyama alichofanyiwa.
********
JESHI
la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa halitavumilia kuona baadhi
ya vikundi vya watu vitakavyoshawishi vurugu au kujianda kuchukua sheria
mkononi kwa kutumia mwamvuli wa tukio la kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Kamishna wa Kanda hiyo Suleimani Kova amesema kuwa kuna baadhi ya watun
wameanza kulichukulia tukio hilo katika kuazisha vurugu na hasa kulishirikisha
na masuala ya kidini jambo ambalo halina ukweli ndani yake.
Amesema kuwa jeshi hilo limemuweka chini ya ulinzi
Sheikh Ponda akiwa katika matibabu kwa kuangalia usalama wake lakini pia ni
kutokana na kuhitajika kwa mahojiano na jeshi la polisi mkoani Morogoro ambapo
lilitaka kumkamata kabla ya kujeruhiwa.
Wakati huohuo jeshi hilo limetangaza zawadi ya
shilingi milioni mia moja kwa mwananchi yoyote ambaye atafanikisha kukamatwa
kwa mtandao wa watu wanaotumia tindikali kujeruhi baadhi ya watu.
12-AUG-KOVA
TINDIKALI.
Aidha jeshi hilo pia limefanikiwa kumkamata Raia
mmoja wa Uingereza ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Trans Africans logstics limited – TALL Bwana
Robert Dewar akiwa na nyara mbalimbali
za Serikali zenye thamani ya zaidi ya shilingi million mia moja kumi na nane.
12-AUG-KOVA
NYARA
No comments
Post a Comment