Promosheni ya miliki biashara ya bajaji na TIGO yaanza kushika kasi,washindi watatu watangazwa,kupewa bajaji zenye thamani ya mamilion
Na Selemani Ahamadi
Kampuni ya simu ya Tigo Imeanza kutoa bajaji zake kwawateja ambao wamefanikiwa
kushinda katika droo iliyochezeshwa katika siku za Ijumaa,Jumamosi na jumapili
ambapo jumla ya washindi watatu wametangwazwa ambapo kila mmoja ameibuka na
bajaji moja yenye thamani ya Tsh. Milioni 6 na laki 7
Akiwatangaza washindi hao meneja chapa wa Tigo, Bw, William
Mpinga amewataja washindi hao kuwa ni pamoja na Mohammedi Ramadhani Mnjore
mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Kondoa ambaye ni mfanya biashara wa nguo huko
Ilala,Mwana Mnjore amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo iliyochezeshwa siku
ya Ijumaa ambapo jumla ya Namba 953,369 zilishindanishwa na ndipo namba yake
ikafanikiwa kushinda
| Wanahabari wakisikiliza kwa makini toka kwa meneja huduma wa tigo |
Mwingine ni Riziki lucas mwenye umri wa miaka 36
anayejishughulisha na kazi ngumu hapa jijini Daresalaam,Bw. Lucas amefanikiwa
kushinda bajaji katika droo iliyochezeshwa siku ya jumamosi ambapo jumla ya
namba 936,860 zilishindanishwa na ndipo
namba ya Riziki Lucas imefanikiwa kuibuka mshindi
Na mshindi wa siku ya tatu ni Bw.Adam Said mwenye umri wa
miaka 36 mkazi wa huko Temeke ambapo naye amefanikiwa kujishindia bajaji,droo
kwa siku ya jumapili ilishindanisha jumla ya wateja 893,437 ambapo yeye
amefanikiwa kushinda katika droo hiyo
Washindi hao waliwashukuru kampuni ya tigo kwa kuendelea
kuwajali wateja wake kwa kuwafanya waweze kumiliki biashara zao wenyewe kwani
kufanya hivyo ni dalili za kuonyesha wazi kuwa tigo inawapenda wateja wake
| Bw. mpinga akichezesha droo ya Ijumaa ambapo Mnjore aliibuka kidedea,,kushoto kwake meneja huduma wa tigo Bw.Husni seif |
PROMOSHENI ya shinda bajaji miliki biashara yako
inayoendeshwa na kampuni ya tigo imezinduliwa hivi karibuni na kwamba kila siku
wateja wa tigo watapata fulsa ya kujishindia bajaji moja kwa kila droo hivyo
wateja wanashauriwa kuendelea kutumia mtandao wa tigo na kuongeza salio lisilo
chini ya shilingi elfu moja tu
Akizungumza na fullhabari
MENEJA HUDUMA WA Tigo Bw.Husni Seif amesema hakuna tozo yeyote inayotozwa
kwa washiriki wa promosheni ya miliki biashara yako na kwamba kujiunga ni bure
kwa wateja wote wa tigo, anachotakiwa mteja ni kuongeza salio lisilochini ya
kiasi cha shilingi 1000 ili kuweza kuingia moja kwa moja na kwamba haingaliwi
kama ulikuwa na deni au la
Ameongeza kusema kuwa wateja ni vema wakachangamkia fulsa
hii iliyojitokeza ili waweze kumiliki biashara zao wenyewe kwani kufanya hivyo
kutawaongezea kipato kwani utafiti unaonyesha biashara hiyo ya Bajaji inalipa
kwa kiasi kikubwa mno
| Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini namna washindi wa bajaji wakitangwazwa |
JUMLA ya bajaji sitini zitatolewa kila siku na droo itachezeshwa kila jumatatu
ambapo jumla ya washindi saba watatangazwa na kuzawadiwa pikipiki zao za miguu
mitatu zenye thamani ya shilingi milion 7na laki tano
| Bw. Mpinga akimsikiliza mmoja wa washindi waliofanikiwa kushinda bajaji |
| Meneja huduma wa TIGO akichezesha droo ya shinda bajaji miliki biashara yako, jumla ya bajaji tatu zimetolewa kwa washindi wa siku ya ijumaa,jumamosi na jumapili |
| Laptop ikichezehsa droo ya shinda bajaji,washindi watatu leo wamejishindia bajaji zenye thamani ya miliion 6.5 |
No comments
Post a Comment