Zinazobamba

Promosheni ya miliki biashara ya bajaji na TIGO yaanza kushika kasi,washindi watatu watangazwa,kupewa bajaji zenye thamani ya mamilion




Na Selemani Ahamadi
Kampuni ya simu ya Tigo Imeanza kutoa  bajaji zake kwawateja ambao wamefanikiwa kushinda katika droo iliyochezeshwa katika siku za Ijumaa,Jumamosi na jumapili ambapo jumla ya washindi watatu wametangwazwa ambapo kila mmoja ameibuka na bajaji moja yenye thamani ya Tsh. Milioni 6 na laki 7
Akiwatangaza washindi hao meneja chapa wa Tigo, Bw, William Mpinga amewataja washindi hao kuwa ni pamoja na Mohammedi Ramadhani Mnjore mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Kondoa ambaye ni mfanya biashara wa nguo huko Ilala,Mwana Mnjore amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo iliyochezeshwa siku ya Ijumaa ambapo jumla ya Namba 953,369 zilishindanishwa na ndipo namba yake ikafanikiwa kushinda
Brand manager wa Tigo Bw. William Mpinga katikati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya promosheni ya BAJAJI ambapo wateja wa tigo wanajishindia bajaji kila siku,wateja wa TIGO wananingia moja kwa moja baada ya kuweka salio lisilo chini ya shilingi elfu moja 1000. Kulia kwake ni meja huduma wa tigo Bw.Husni Seif na Game inspector Chiku salehe toka bodi ya serikali ya bahati nasibu



Wanahabari wakisikiliza kwa makini toka kwa meneja huduma wa tigo



Mwingine ni Riziki lucas mwenye umri wa miaka 36 anayejishughulisha na kazi ngumu hapa jijini Daresalaam,Bw. Lucas amefanikiwa kushinda bajaji katika droo iliyochezeshwa siku ya jumamosi ambapo jumla ya namba  936,860 zilishindanishwa na ndipo namba ya Riziki Lucas imefanikiwa kuibuka mshindi
Na mshindi wa siku ya tatu ni Bw.Adam Said mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa huko Temeke ambapo naye amefanikiwa kujishindia bajaji,droo kwa siku ya jumapili ilishindanisha jumla ya wateja 893,437 ambapo yeye amefanikiwa kushinda katika droo hiyo
Washindi hao waliwashukuru kampuni ya tigo kwa kuendelea kuwajali wateja wake kwa kuwafanya waweze kumiliki biashara zao wenyewe kwani kufanya hivyo ni dalili za kuonyesha wazi kuwa tigo inawapenda wateja wake

Bw. mpinga akichezesha droo ya Ijumaa ambapo Mnjore aliibuka kidedea,,kushoto kwake meneja huduma wa tigo Bw.Husni seif
PROMOSHENI ya shinda bajaji miliki biashara yako inayoendeshwa na kampuni ya tigo imezinduliwa hivi karibuni na kwamba kila siku wateja wa tigo watapata fulsa ya kujishindia bajaji moja kwa kila droo hivyo wateja wanashauriwa kuendelea kutumia mtandao wa tigo na kuongeza salio lisilo chini ya shilingi elfu moja tu

Akizungumza na fullhabari  MENEJA HUDUMA WA Tigo Bw.Husni Seif amesema hakuna tozo yeyote inayotozwa kwa washiriki wa promosheni ya miliki biashara yako na kwamba kujiunga ni bure kwa wateja wote wa tigo, anachotakiwa mteja ni kuongeza salio lisilochini ya kiasi cha shilingi 1000 ili kuweza kuingia moja kwa moja na kwamba haingaliwi kama ulikuwa na deni au la

Ameongeza kusema kuwa wateja ni vema wakachangamkia fulsa hii iliyojitokeza ili waweze kumiliki biashara zao wenyewe kwani kufanya hivyo kutawaongezea kipato kwani utafiti unaonyesha biashara hiyo ya Bajaji inalipa kwa kiasi kikubwa mno

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini namna washindi wa bajaji wakitangwazwa
JUMLA ya bajaji sitini zitatolewa  kila siku na droo itachezeshwa kila jumatatu ambapo jumla ya washindi saba watatangazwa na kuzawadiwa pikipiki zao za miguu mitatu zenye thamani ya shilingi milion 7na laki tano
Bw. Mpinga akimsikiliza mmoja wa washindi waliofanikiwa kushinda bajaji









Meneja huduma wa TIGO akichezesha droo ya shinda bajaji miliki biashara yako, jumla ya bajaji tatu zimetolewa kwa washindi wa siku ya ijumaa,jumamosi na jumapili

Laptop ikichezehsa droo ya shinda bajaji,washindi watatu leo wamejishindia bajaji zenye thamani ya miliion 6.5

No comments