MWANYA AWA BALOZI WA VIN NKOLOMBOKA.
Na Mwandishi Wetu.
Msanii na mchekeshaji maarufu nchini Mwanya,amepewa ubalozi rasmi wa kinywaji cha asili cha Vin Nkolomboka,ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kukuza bidhaa za ndani na kuongeza wigo wa soko lake nchini.
Akizungumza Oktoba 22,2026 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simba Beverages Limited Tanzania(SBL)ambayo inazalisha kinywaji hicho Bw.Roy amesema kuwa wameamua kumtumia Mwanya kama balozi kwani amekua akifanya vizuri katika tasnia ya uchekeshaji hapa nchini.
"Tunalenga kutumia umaarufu wa Mwanya katika tasnia ya uchekeshaji kuhamasisha wananchi kukitambua kinywaji chetu kinachozalishwa na kampuni yetu kupitia kiwanda chetu kilichopo wilayani Kibaha,Mkoani Pwani."amesema Roy
Nakuongeza "Mwanya ana uwezo wa kuleta furaha na burudani kwa jamii, sifa zinazolingana na falsafa ya bidhaa hiyo inayohusishwa na kauli mbiu ya “Good Vibe with Good Health.”
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo kinywaji cha Vin NKolomboka hutengenezwa kwa kutumia viungo vya asili vinavyojumuisha tangawizi, pilipili manga,asali na sukari, ambavyo huchachushwa ili kuzalisha kinywaji chenye kilevi,Kinywaji hicho kimeelezwa kuwa na kiwango cha pombe cha asilimia 12.

Kwa upande wake Mwanya ameonesha hali ya kafurahishwa na hatua hiyo, huku akiahidi kushirikiana na kampuni hiyo katika shughuli za utangazaji na kukuza uelewa wa bidhaa hiyo kwa wananchi.
Amesema kuwa kupitia ushirikiano huo, kampuni inatarajia kuimarisha kampeni za masoko na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza upatikanaji wa Vin NKolomboka katika maeneo tofauti nchini.


No comments
Post a Comment