Zinazobamba

TAKUKURU ILALA YASHIRIKI KONGAMANO LA 4 LA KITAIFA LA HUDUMA ZA MAKTABA,TAMASHA LA VITABU NA USOMAJI.

Na Mwandishi Wetu.Dar es salaam 

Dar es Salaam.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala imeshiriki katika Kongamano  la 4 la Kitaifa la Huduma za Maktaba, Tamasha la Vitabu na Usomaji.

Akizungumza leo Oktoba 21,2026 na waandishi wa habari katika kongamano hilo linalofanyika Jijini Dar es Salaam,  Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Bi.Immaculate Ngoti 

amesema lengo la kushiriki Kongamano hilo    ni kuendeleza ushirikiano na wad mbalimbali wakiwemo Bodi ya Taifa ya Huduma za Maktaba na kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa na madhara yake.

Bi.Ngoti amesema pia lengo ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya nafasi ya maktaba katika kukuza maarifa, Maadili na maendeleo ya Taifa, kuweka mikakati ya kuzifanya maktaba ziwe na tija na za kisasa na zisizo na Rushwa ikienda sambamba na  kutoa elimu na kupokea kero mbalimbali zinazohusiana na  Rushwa katika utoaji wa Huduma kwa Jamii.Afisa huyo mesema  ni jukumu lao kushirikiana na jamii katika kuzuia na kupambana na rushwa kwakuwa ni moja ya majukumu yao ya kilasiku katika jamii.

"Sisi tunahamasisha wananchi wote juu ya matumizi mazuri ya maktaba kwakuwa maktaba si sehemu ya kuhifadhi vitabu tu,bali ni kituo cha kupambana na ujinga, umaskini na rushwa kwa  kutoa taarifa sahihi"Alisema Bi Ngoti.Aidha Bi.Ngoti ametoa wito kwa jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa na kuiomba jamii kufika katika banda la Takukuru inapofanyika kongamano hilo la 4 la kitaifa la  huduma za maktaba,Tamasha la vitabu na usomaji katika viwanja vya huduma ya bodi ya maktaba jijini Dar es Salaam.



No comments