Zinazobamba

Maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani ngazi ya jamii

Sauti ya jamii jamii Kipunguni kwa kushirikiana na kamati ya Mtakuwa mtaa wa Amani pamoja na wadau wengine waadhimisha siku ya Vijana kwa kuwaleta pamoja Vijana zaidi ya 250 kujadili fursa, vikwazo na nini kifanyike

Mafunzo mbalimbali yanatolewa ikiwemo Elimu ya Afya ya akili, Uzalendo, Afya ya uzazi, uchumi na umuhimu wa Vijana kushiriki kuzuia Ukatili wa kijinsia. 

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kutoa zawadi ya Mbuzi kwa Mkuu wa Upelelezi kituo cha Polisi Kivule kutokana na kazi nzuri anayoifanya kuzuia uhalifu kwenye jamii. 

Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo kaimu Mwenyekiti wa Sauti ya Jamii Kipunguni bi. Tausi Msangi amesema wameamua kuwaleta pamoja Vijana kwa sababu wanaijua nguvu ya Vijana katika kuzuia Ukatili 

"Sisi kama sauti ya jamii Kipunguni tunaamini katika nguvu ya pamoja katika vita dhidi ya ukatili na tunaelewa Vijana wanavyopitia mengi yanayosababisha msongo wa mawazo ikiwemo mahusiano ya uongo (fake) hivyo elimu ya Afya ya akili ni muhimu Sana kwao". 

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Amani ndugu Abdi Mahanyu amesema miezi minne iliyopita kulikuwa na wimbi la wizi kwenye mtaa wa Amani lakini kwa kushirikiana na mkuu wa Upelelezi kituo cha polisi Kivule wamepunguza tatizo hilo kwa asilimia kubwa sana na ndio maana wanajamii wamechanga na kumnunulia mbuzi ikiwa ni kutambua mchango wake. 

Mwakilishi wa Vijana ndugu Ikram Mnyani amesema wanashukuru Sana kuletwa pamoja na kupewa Elimu ya Afya ya akili na Afya ya uzazi "leo nimepata kitu kipya elimu hii ya msongo wa mawazo imeniingia Sana Vijana wengi tunateseka na mahusiano kusema ukweli leo nimepata ahueni na nitaenda kusambaza elimu hii kwa wenzangu".

Afisa maendeleo ya jamii kata ya Kipunguni bi Rozina soka amehimiza Vijana kujiunga kwenye Vikundi ili iwe rahisi kufikiwa fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya halmashauri.

Afisa maendeleo kata ya Kipunguni bi Rozina soka akiongea na Vijana kwenye maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika mtaa wa Amani Kipunguni
Wanajamii wa mtaa wa Amani kata ya Kipunguni wakimkabidhi zawadi ya mbuzi mkuu wa Upelelezi kituo cha police Kivule (mwenye tishrt nyeupe) kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kupunguza uhalifu.
Afisa maendeleo kata ya Kipunguni bi Rozina soka akiongea na Vijana kwenye maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika mtaa wa Amani Kipunguni
Afisa ustawi wa jamii Tumaini Urio akitoa elimu ya Afya ya akili kwenye maadhimisho ya Vijana Duniani yaliyofanyika mtaa wa Amani Kipunguni.

No comments