Zinazobamba

DIB YAFANIKIWA KUPUNGUZA MIGOGORO YA UENDESHAJI WA TAASISI ZA KIFEDHA, BALOZI DR.OMARI AIPONGEZA


Na Mussa Augustine

Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Joyce Shala, amesema bodi hiyo imefanikiwa kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika uendeshaji wa taasisi za kifedha nchini.

Shala amesema hayo leo Julai 2,2026 wakati Waziri wa Fedha, Balozi Dr. Khamis Mussa Omar, alipotembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa.Amesema DIB imefanikiwa kuwalipa wateja wa iliyokuwa Benki ya FBME kwa asilimia 85, ambapo katika awamu ya kwanza walilipwa asilimia 35, awamu ya pili asilimia 28 na awamu ya tatu asilimia 35.

Katika ziara hiyo, Balozi DR.Omar alipokelewa na viongozi pamoja na wafanyakazi wa DIB na kupatiwa maelezo kuhusu majukumu ya bodi hiyo, huduma inazotoa pamoja na jitihada zinazoendelea kufanywa katika kutoa elimu kwa umma kuhusu Mfumo wa Bima ya Amana.Aidha, Balozi Omar alipata fursa ya kufahamu mchango wa DIB katika kulinda amana za wateja wa benki na taasisi za fedha, sambamba na kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha nchini.

No comments