Na Mwandishi wetu.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) kushirikiana na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) limeungana kuanzisha kutoa tuzo za waandishi wa habari wanaoelimisha jamii kuhusiana na changamoto, matukio ya hali mbaya ya hewa na tahadhari zitokana na usalama kwenye majiAfisa Uchechemuzi kutoka Shiriki la Usimamizi wa Mazingira na maendeleo(EMEDO) Mary Francis Mahemba amesema, wametambua mchango unaofanywa na vyombo vya habari kuwa ni muhimili muhimu katika kuifikia jamii kutoa taarifa sahihi zitakazoweza kuokoa maisha, kupunguza athari za majanga yanayohusianana hali ya hewa pamoja na kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu usalama wa majini.

Amefafanua tuzo hizo zinalenga kuhasamasisha utayarishaji wa habari zenye ubora kuhusu matukio ya hali mbaya ya hewa na athari zake kwa jamii, tahadhari za mapema za hali ya hewa, usalama wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kwenye maji, uzuiaji wa ajali na vifo vitokanavyo na kuzama maji, pamoja na ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga yanayohusiana na hali ya hewa.

Tuzo hizo zitahusisha waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii, redio, magazeti, Televisheni na majukwaa ya kidijitali nchini.Kwaupande wake Meneja Masoko na Uhusiano kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, Monica Mutoni amesema umuhimu wa taarifa za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari za mapema pamoja na kuokoa maisha ya wananchi hususani wale wanaotegemea shughuli za maji kama vile wavuvi na usafiri wa majini.

Ushirikiano katika tuzo hizo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma, mashirika ya kiraia na vyombo vya habari katika kuimarisha uelewa, usambazaji wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika shughuli zote za kiuchumi na kijamii.