MTOTO WA HAYATI BABA WA TAIFA ASHINDA KWENDA WORLD CUP CANADA NA CRDB TEMBOCARD VISA
Kupitia droo kubwa ya FIFA World Cup 2026 “Fainali Ndiyo Mpango na Tembo Card Visa” iliyochezeshwa na CRDB mapema leo, mtoto wa Hayati Mwalimu Nyerere aitwaye Charles Makongoro Nyerere ameibuka mshindi baada ya kupigiwa simu mubashara, ikiwa ni matokeo ya kutumia CRDB katika matumizi ya fedha.
Ambapo amepewa taarifa kuwa ameshinda droo ya kwenda nchini Canada kuangalia fainali za Kombe la Dunia 2026.
CRDB imechezesha droo ya pili ya kusaka washindi wa kwenda Marekani, Canada na Mexico kuangalia mashindano ya fainali za Kombe la Dunia, mashindano makubwa zaidi ya soka kwa timu za taifa duniani.
Kampeni hiyo imepewa jina la FIFA World Cup 2026 “Fainali Ndiyo Mpango na Tembo Card Visa”, ambapo imepata washindi watatu wa TV Janja nchi 85 na washindi watatu walioshinda kwenda Canada.

No comments
Post a Comment