Boxing Media Day kufanyika April 15 mwaka huu.
Na Mussa Augustine.
Chama Cha Makocha wa Ngumi za kulipiwa Tanzania(TPBRC)kinatarajia kufanya Media Day April 15 mwaka huu kwa kutembelea sehemu za mazoezi ya Ngumi(Gym).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 30,2026 Mwenyekit wa chama hicho Jaffary Ndame amesema kuwa siku hiyo itakua muhimu kwa kutangaza kazi zinazofanywa na walimu wa masumbwi pamoja na kazi za chama kwa ujumla.
Aidha amesema kwamba lengo la chama hicho ni kutokana n akua kiini Cha Boxing Nchini Tanzania,hivyo Wana dhamira n amalengo makubwa ya kuongeza taaluma kwa Makocha na Kukuza mabondia ambao wanaweza kulitea heshima ya Ngumi Tanzania,
"Sisi walimu wa Ngumi za kulipiwa tunasubira matunda makubwa sana kutokana na kazi yetu tunayoifanya ya kufundisha mabondia."amesema Ndame.
Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Jumma Mbogo ametambulisha kamati mbalimbali ambazo zitafanikisha katika siku ya Boxing Media Day kuwa ni pamoja na kamati ya ufundi,kamati ya Nidhamu,kamati Afya,pamoja kamati ya habari na Mawasiliano.
Aidha amesema kwamba boxing media day imedhaminiwa na Robby Farmer's ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini ili kukuza sekta ya Ngumi za kulipiwa.
Akizungumza mweka hazina wa Hamis Richard amesema kuwa chama hicho kitahakikisha walimu wa mabondia wananufaika na mikataba ili kuweza kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini.
Nae Meneja wa habari Mawasiliano Somba Dauka amesema kuwa Robby Farmers wameandaa zawadi zitakazotolewa kwa mabondia wanawake kwenye sehemu za mazoezi(Gym)zonazofundishwa na Makocha wanawake


No comments
Post a Comment