MKUTANO WA KAMATI TENDAJI CAF KUFANYIKA FEBRUARI 13 MWAKA HUU NCHINI TANZANIA.
Na Mussa Augustine.
Mkutano Mkuu wa Kamatitendaji ya Shirikisho la mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF)unatarajiwa kufanyika Februari 13 mwaka huu katika ukumbi Hayyat Regency Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa leo Februari 9,2026 na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Paul Makonda wakati akizungumza na Waandishi wa habari.
"Ikumbukwe tarehe 16 mwezi wa kwanza ,Dkt. Samia Suluhu Hassan alituma ujumbe maalumu kwenda kwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Afrika(CAF) Patrice Motsepe ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa ambao anatoa kwenye mpira wetu wa miguu barani Afrika na kwanamna ambavyo amechagiza kuinua vipaji na kuleta amani kwa Vijana wetu.
Nakuongeza kuwa" ujumbe huo maalumu kulikuwepo mambo mengi mahsusi ikiwemo Dkt Samia Suluhu Hassan kumuonesha Rais wa CAF namna gani yupo Tayari kuwekeza kwa gharama yoyote kuhakikisha Tanzania hapo baadae inakua kinara wa Michezo barani Afrika hada Dunia kwa Ujumla.
Ndugu yetu Motsepe amepokea ujumbe wa DktSamia kwa uzito mkubwa,yapo mambo ambayo tulijadiliana ikiwemo ni pamoja na CAF kufanya mikutano yake ya Mwaka ndani ya Tanzania.
Aidha Waziri Makonda amesema kuwa hali hiyo itatoa fursa ya kwa kiongozi huyo kuona maendeleo na uwekezaji mkubwa ambao Dkt Samia anaufanya.
"Rais Motsepe ameridhia kuja kufanya Mkutano wake na kamati tendaji,na leo tarehe 9 timu yake ya sekretarieti imeanza kuingia nchini,na mkutano wao Mkuu utafanyika tarehe 13.mwezi huu." Amesema Waziri Makonda

No comments
Post a Comment