Zinazobamba

CCM TEMEKE YAJIVUNIA MAENDELEO MAKUBWA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA CHAMA HICHO.

Na Mwandishi wetu

Ikiwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinaadhimisha Miaka 49 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977,Chama hicho kimefanya maendeleo makubwa katika Wilaya ya Temeke katika Sekta ya miundombinu ya Barabara,Afya na Elimu.

Hayo yamesemwa leo Februari 4,2026 na Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Daniel Sayi wakati akizugumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, kuelekea maadhimisho hayo yatakayofanyika siku ya alhamisi ya Februari 5,2026.

Aidha amesema kuwa chama hicho tangu kipate ridhaa ya kushika Dola kimeendelea kutekeleza Ilani yake kuwaletea maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali.

"Chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Ilani ya CCM inatafsiriwa katika kiwango cha kimkoa na wilaya,sisi tunafuraha kwenye Wilaya yetu ya Temeke kazi ya kutekeleza Ilani ya chama chetu inaendelea vizuri katika sekta mtambuka"amesema Bw.Sayi

Amesema kuwa kufikia miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama hicho,kinaamini katika usawa wa kibinadamu na kuishi katika misingi ya Amani,Umoja, Utulivu na Mshikamano kwani ndio tunu za Taifa,pamoja nakujivunia kwa kazi zilifonywa tangu nchi ipate uhuru.

Aidha ameendelea kusema kuwa miradi ya barabara inaendelea kutekelezwa Wilayani humo ili kufanya Mapinduzi makubwa ya miundombinu ya barabara.

"Miundombinu ya barabara inapokuwa vizuri urahsi wa maisha ya watanzania unakuwa wepesi"amesema 

Ameongeza kuwa mradi mpya wa mabasi yaendayo haraka unaotekelezwa wilayani Temeke umekuwa chachu ya Maendeleo kwa wafanyabiashara pamoja na Wananchi kwa ujumla.

"Ndani ya siku 100 za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,mradi huu wa mabasi ya mwendokasi umeendelezwa zaidi na kuwa na ufanisi mkubwa kiuchumi kwa wananchi wa mbagala na maeneo mengine ya karibu "amesema 

Kwa upande wa sekta ya Afya,Bw.Sayi amesema hospitali na zahanati zimeendelea kuboreshwa zaidi ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba nakwamba Wananchi wanapata huduma bora.

"Malalamiko ya kuzuiliwa kwa miili ya watu wanaofariki dunia kwa sasa malalamiko hayo hayapo toka Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atoe ahadi ya kushughulikia suala hilo,hivyo hapa Ofisini kwasasa hatujapokea  malalamiko yoyote"amesema 

Bw.Sayi ameendelea kueleza kuwa kwa upande wa sekta ya elimu,miradi ya kujenga shule mpya za hadhi ya ghorofa za kisasa zaidi unaendelea  kutekelezwa nakuondoa adha mbalimbali ikiwemo upungufu wa madarasa.

Hata hivyo Katibu huyo amewasihi wananchi kuwapuuza wale wote wanaotoa kauli za uchochezi ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa Amani kwa Taifa. 

No comments