MAHAFALI YA SITA YA TIPM YAMEACHA KUMBUKUMBU YA KUDUMU.
Na Mwandishi Wetu.
Chuo cha Usimamizi wa Miradi Tanzania (TIPM) kimefanya Mahafali yake ya Sita ambayo yamefanyika kwa heshima kubwa na kuacha kumbukumbu ya kudumu kwa wahitimu pamoja na wageni waliohudhuria.
Mahafali hayo yalifanyika Januari 31, 2026 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, ambapo wahitimu walionekana wakiwa wamejaa fahari na shangwe wakati wa hafla hiyo muhimu ya kihistoria.
Wahitimu hao waliingia katika ukumbi wa mahafali kwa maandamano ya kuvutia yaliyoongozwa na Bendi ya Shaba (Brass Band), hatua iliyoongeza hadhi, utulivu na mvuto wa tukio hilo. Muziki wa bendi hiyo uliakisi mshikamano, mafanikio na kilele cha miaka ya bidii na juhudi za kitaaluma.
Katika hafla hiyo, wahitimu walipokelewa rasmi na kufuatiwa na zoezi la utoaji wa vyeti, lililotambua juhudi, nidhamu na ubora wao wa kitaaluma. Furaha, makofi na shangwe kutoka kwa familia, wakufunzi pamoja na wageni walioalikwa vilitawala katika hafla hiyo.
Aidha, mahafali hayo yataendelea kukumbukwa kama kielelezo cha dhamira, ubora na weledi unaojengwa na Chuo cha TIPM kwa wahitimu wake.
Reviewed by mashala
on
19:40:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment