Zinazobamba

MKAKATI WA TAIFA UMELENGA KUFIKIA 80% YA WATANZANIA KUTUMIA NISHATI SAFI IFIKAPO 2034


*📌Kutoa uelewa kwa Watanzania kuhusu Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia*

*📌Kuwashirikisha Wadau mbalimbali ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa kwa bei nafuuu hususani maeneo ya Vijijini*

Dar es salaam

Imeelezwa Kuwa, Mkakati wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia ni Dira muhimu ya kufanikisha malengo ya Taifa ya kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi na salama, rafiki wa mazingira na yenye gharama nafuu hadi kufikia mwaka 2034 ambapo asilimia 80% ya Watanzania wawe wanatumia  nishati safi ya kupikia.

Hayo yamebainishwa leo novemba 17, 2025 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati Bi. Neema Mbuja wakati akizungumza  na wananchi katika kipindi cha Crown Sport Jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa Mkakati wa Nishati safi ya kupikia ni nyenzo muhimu katika kutekeleza makubaliano ya kitaifa na kimataifa yanayolenga kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kupunguza uzalishaji wa gesi joto.   

“Kupitia Mkakati wa Taifa wa miaka kumi, Serikali inalenga kufikisha asilimia 80 ya kaya za Tanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Mkakati huu unajikita katika kupunguza magonjwa ya kupumua yanayotokana na moshi, kulinda misitu, na kuongeza fursa za kiuchumi kupitia uwekezaji katika teknolojia na vifaa safi vya kupikia pia Serikali imesisitiza kuwa utekelezaji wa mkakati huo utahusisha sekta binafsi, taasisi za maendeleo, na jamii kwa ujumla zinazolisha watu zaidi ya 100 kama Shule na Magereza”. Ameeleza Bi. Mbuja.

Amefafanua kuwa, Mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia unakwenda sambamba na Mkakati wa mawasiliano kwani umelenga kuamsha uelewa wa watanzania  kupata taaarifa juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia siliano kwani kupitia kampeni za kitaifa zitakazohusisha redio, televisheni, mitandao ya kijamii, maonyesho ya wazi, pamoja na mafunzo maalum kwa viongozi wa jamii, waandishi wa habari na washawishi wa mitandaoni  Watanzania wanapata ujumbe mahususi na uelewa  kuhusu nishati safi ya kupikia.Kwa upande wake, Mhandisi wa Utafiti Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Samwel Kessy ameeleza kuwa Mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia ni dhana muhimu ya kufanikisha malengo ya Taifa ya kuhakikisha usalama, uendelevu na urahisi wa upatikanaji wa nishati  safi ya kupikia, kuokoa muda, pamoja na kupunguza gharama za matumizi, athari za kimazingira na kiafya kwa watumiaji.

Ameongeza kuwa, Serikali  ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha kila Mwananchi anapata uelewa juu ya faida za matumizi ya  nishati safi ya kupikia pamoja na kuhakikisha wadau mbalimbali wanashirikishwa ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa na nishati kwa bei nafuu, hususan imaeneo ya vijijini.“Sisi kama TANESCO tumehakikisha umeme umewafikia wateja kwa kiasi kikubwa na unapatikana kwa uharaka lakini pia kwa kushirikiana na sekta binafsi tumehakikisha wananchi wanapata vifaa bora vya kupikia na vyenye gharama nafuu ili waweze kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia. Amesisitiza Mhandisi. Kessy.



No comments