KIONGOZI RAI APONGEZA TAMISEMI KUPELEKWA OFISI YA WAZIRI MKUU.
Rashid Rai akizungumza kwenye moja ya Mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025(picha na AAFP)
Na Mussa Augustine.
Pongezi hizo amezitoa leo Novemba 18,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu,nakubainisha kwamba hatua hiyo itarahisisha kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Aidha Kiongozi Rai amesema kuwa TAMISEMI kupelekwa Ofisi ya Waziri Mkuu itasaidia kurahisisha ugatuzi wa madaraka na kuwafanya watendaji wafanye kazi kwenye maeneo yao bila kuingiliana kiutendaji.
Pia amesema kuwa hatua hiyo itamsaidia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG)kufanya kazi yake kwa ufanisi na kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa bila kuwepo na ubadhilifu wa fedha za umma.
"Hili suala,AAFP tumelipigia kelele sana,hata kipindi cha kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita,tumelipigia kelele sana,kwa vile Rais Dkt.Samia ameona umuhimu wake nakuchukua hatua,mimi binafsi(Rashid Rai)na kwa niaba ya chama changu tunampongeza sana sana kwa kuchukua hatua hiyo" amesema kwa furaha kiongozi huyo wa AAFP.
Ikumbukwe kuwa Novemba 17,2025 Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan alitangaza rasmi Baraza lake jipya la mawaziri pamoja na kufanya madiliko ya baadhi ya Wizara ikiwa lengo ni kuongeza ufanisi wa utendaji wa Serikali katika kutatua changamoto za Wananchi pamoja na kuwaletea maendeleo.

No comments
Post a Comment