Zinazobamba

MGOMBEA URAIS AAFP KUTEMBEA NA WAKULIMA,WAFUGAJI NA WALIMU.

Na Mwandishi Wetu. Mvuha Morogoro.

"Kwenye Serikali yangu ya awamu ya saba,nitatembea pamoja na Wakulima,Wafugaji na Walimu kwasabubu ni watu muhimu sana kwenye Taifa letu".

Ni matamshi yaliyotolewa leo Septemba 1,2025 na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP) Kunje Ngombale Mwiru wakati akihotubia Wananchi  wa kata ya Mvuha Wilayani Morogoro Mkoani Morogoro,katika kampeni za Urais zinazoendelea Mkoani humo.

Aidha Mgombea huyo amesema kuwa Wakulima wa kata ya  Mvuha na maeneo mengine wamekua hawana soko la uhakika kuuza mazao yao huku vyama vya ushirika AMCOS Wilayani humo vikiendelea kununua mazao yao kwa bei ya chini kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani.

Ameendelea kusema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi,Serikali yake itahakikisha inavifuta vyama vyote vya ushirika kwani vimekua vikiwanyonya Wananchi kwa kununua mazao kwa bei isiyo na manufaa.
Kuhusu Wafugaji, Mheshimiwa Mwiru amesema kuwa atahakikisha wanatengewa  maeneo mazuri ya kufanya shughuli za ufugaji bila kuingia kwenye maeneo ya Wakulima,pamoja na kuwepo kwa soko la uhakika la kuuza mifugo yao.

Akizungumzia kada ya ualimu Mgombea huyo amesema kwamba walimu wanapaswa kuheshimiwa kwani ndio wanaozalisha Wataalamu ambao wanafanya kazi katika sekta mbalimbali nakuleta maendeleo kwa Taifa.
Hata hivyo amesikitishwa na hali ya Wananchi wa Kata ya Mvuha kutumia Maji yasio salama kwa afya zao kutokana na maji ya Mto uliyopo maeneo hayo  kutumika kuchenjua Madini ambapo Maji hayo ndio wanatumia Wananchi kunywa na kupikia hali inayohatarisha maisha yao.

"Inasikitisha sana Wananchi mnakunywa Maji machafu na Serikali ipo inaangalia tu,Afisa Mazingira yupo anaagalia, maisha yenu yapo hatarini kwa kupata mgonjwa ya saratani kutokana na kemikali zinazotumika kusafisha madini,hivyo ni muda wenu sasa kutumia uchaguzi wa Oktoba Mwaka huu kubadilisha Serikali,iliyopo madarakani imeshindwa kuwatumikia" amesema Mwiru.
Kwa upande wake Mgombea Mwenza Chumu Abdallah amesema kuwa  Muda wa mabadiliko ni sasa,hivyo Wananchi wajitokeze kwa wingi kukipigia kura chama Cha AAFP kuanzia nafasi ya Udiwani,Ubunge na Urais ili kuweza kupata maendeleo ya kweli.

Nae Katibu Mkuu AAFP Taifa Rashid Rai ameonesha kuchukizwa na kitendo Cha kuwasilisha barua ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro mgombea ubunge Jimbo la Morogoro Kusini wa Chama hicho nakuitaka TAKUKURU kuchungza Mazingira yaliyopelekea kufikia uamuzi huo.
"Naiomba TAKUKURU ifanye uchuguzi haraka kuhusiana na kitendo hiki,haiwezekani Mgombea wetu ajiondoe dakika za mwisho,kuna viashiria vya rushwa" amesema Rai.

Nakuongeza kuwa" Tume huru ya uchaguzi ihakikishe uchaguzi unarudiwa kwenye maeneo yote ambayo itaonekana kuna Mgombea mmoja tu wa CCM,ikitokea hivo lazima uchaguzi mdogo uitishwe kwasababu wagombea wengi wanajitoa kwasababu ya kushinikizwa kwa vitisho au kupewa rushwa. 


No comments