Zinazobamba

KUNJE NGOMBALE MWIRU ASITISHA KAMPENI NYUMBANI KWAO KILWA MASOKO.

*Nikufuatia kuwepo kwa gari aina ya Noah kwenye eneo la mkutano wake yenye picha za mgombea urais wa CCM Samia Suluhu Hassan.

*Katibu Mkuu Rai asema kitendo hicho nikinyume na kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC)ambapo hairuhusiwi kuwepo kwa matangazo yoyote ya chama kingine wakati wa kampeni ya chama fulani.

*Naibu Katibu Mkuu AAFP, pamoja na Mwandishi wa habari wa chombo cha mambo leo tv simu zao zashikiliwa na kupekulilwa na askari Polisi kabla ya kuanza kwa kampeni.


Na Mwandishi Wetu.Kilwa Masoko Lindi.

Mkutano wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima AAFP Wilayani Kilwa Mkoani Lindi umesitishwa ghafla kutokana na kuwepo kwa gari aina ya Noah ambayo ilikua na picha za mgombea urais kupitia CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Gari hiyo yenye namba za  usajili T.181 BST iliegeshwa  katika eneo la stendi ya Kilwa Masoko ambapo  chama cha AAFP kikizindua kampeni zake katika mikoa ya kusini Septemba 19,2025.

Aidha pamoja na viongozi wa AAFP kuwaomba askari polisi waliokua wakilinda usalama wa raia katika eneo hilo hawakuweza kumchukulia hatua dereva wa gari hiyo kwa madai kuwa yeye sio mmiliki wa gari bali kaegesha kwa ajili ya kufanya biashara ya kusafirisha abiria.

Hali hiyo ambayo ilimlazimu Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima AAFP Kunje Ngombale Mwiru kwenda kuamuru dereva wa Noah hiyo kuondoa gari hiyo lakini alionesha ukaindi mbele ya Mgombea huyo huku askari polisi wakishindwa kuchukua hatua yoyote.
Aidha hatua hiyo ilipelekea mheshimiwa Kunje kuahirisha mkutano huo nakuondoka kwenye eneo hilo huku askari polisi wakiwa wamesimama bila kutoa ushirikiano wa aina yoyote. 

Akizungumzia tukio hilo katibu wa AAFP Mkoa wa Pwani aliyekuepo  kwenye kampeni hizo Mariam Mwambusi amesema kwamba kitendo hicho kimevunja kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) hivyo inapaswa askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilwa waliokua wanalinda mkutano huo wachukuliwe  hatua za
 kisheria.
"Ni jambo la aibu sana,hatujafurahi kuona askari polisi wanamuangalia tu dereva kapaki gari lenye picha za mgombea wa chama kingine, hairuhusiwi kufanya hivyo,naomba wachukuliwe hatua inawezekana kuna watu nyuma yao wamewatuma" amesema Mariam Mwambusi ambaye pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Kibiti Mkoani humo.
Naye katibu wa  itikadi na uenezi wa chama hicho Rashid Maokola ameonesha kukasilishwa na kitendo hicho kutokana na kutoa matangazo kwa muda mrefu ili liondolewe gari hilo lakini gari hilo bado lilionekana kuegeshwa katika eneo la mkutano wa kampeni za AAFP. 
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu AAFP Mark Isdori amesema kuwa mzozo wa askari na viongozi wa chama hicho ulianza mapema kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni kwani askari polisi walifikia kwenye eneo hilo nakuwataka kuzima spika za matangazo kwa madai kuwa wananchi wanalalamika kupigiwa kelele,nakwamba hakuna taarifa ya kuwepo kwa mkutano katika stendi ya Kilwa Masoko.

Baada ya katibu mkuu Rashid Rai kufika katika eneo hilo na kukutana na kazia hiyo aliwaonesha askari hao ratiba ya kampeni ya INEC ikionesha AAFP inapaswa kufanya kampeni katika eneo la stendi hiyo ndipo askari wakaruhusu mkutano kuendelea lakini kabla ya kuahirishwa askari hao walionekana kuwa na ushirikiano mdogo kwa viongozi wa AAFP.


No comments