KUNJE RASMI KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA AAFP
Kunje Ngombale Mwiru ameteuliwa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha AAFP ambapo atakua na Mgombea mwenza Chuma Ali.
Wagombea hao wameteuliwa juzi August 27,2025 na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) baada ya kutimiza vigezo na kuidhinishwa kugombea nafasi hiyo,na sasa kinachosubiriwa ni uzinduzi wa kampeni za chama hicho utakaofanyika Septemba 1,2025 Kisaki Mkoani Morogoro.
Kunje Ngombale Mwiru ambaye ni mtoto wa aliyekua mwanasiasa mkongwe hayati Kingunge Ngombale Mwiru,anatarajiwa kufanya siasa za aina yake kwani ana uzoefu mkubwa wa kunadi sera za chama pamoja na masuala yanayohusu uongozi.
Kunje amekabidhiwa gari jipya la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser GX VXR kutoka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)kwa ajili ya kufanya kampeni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai alisema kuwa kampeni za chama hicho zitafanyika Kisaki,Morogoro kwani eneo hilo ndiko chama kilipo asisiwa.
"Tunatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zetu pale Kisaki,Morogoro Vijijini,huko ndiko chama chetu kiliasisiwa,kwahiyo tunashukuru sana tume huru ya uchaguzi kwa kumuidhinisha Mgombea wetu wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kilichobaki sasa ni kuzunguka nchi nzima kuwaeleza Wananchi nini tutawafanyia endapo watatupa ridhaa ya kushika dola"alisema Rai.
Nakuongeza kuwa"Chama chetu kimesimamisha wagombea wa Udiwani na Ubunge katika maeneo mbalimbali Nchini,endapo uchaguzi utakua huru nawa haki tunatarajia kupata ushindi wa kishindo katika maeneo yote tuliyosimamisha wagombea.
Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa gari aina ya Toyota Land Cruiser GX VXR sambamba na madereva wa serikali kwa wagombea Urais pekee ili kusaidia wagombea kufanya kampeni zake kwa urahisi katika maeneo yote.
No comments
Post a Comment