MCHAKATO WA MCHUJO WA WAGOMBEA NDANI YA CCM UNACHUKUA MUDA MREFU KUTOKANA NA UKUBWA WA CHAMA:MBETO
Mchakato wa mchujo wa wagombea wa Ubunge, Uwakilishi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), unachukua muda mrefu kutokana na ukubwa wa chama hicho.
Akizungumza wanahabari Zanzibar jana, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema kuna vikao vingi vinapitia majina ya watia nia.
Alidai kushangaa kuwasikia ACT Wazalendo wakihoji kuchelewa kutangazwa wagombea CCM.
Alisema jana 10 Julai walimaliza vikao ngazi ya mkoa na leo 11 Julai mwaka huu ni zamu ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa.
"Vikao havijafika mwisho, CCM chama kikubwa na hata ndio maana umeona idadi kubwa ya wanachama wamejitokeza kuchukua fomu" alisema Mbeto.
"Makada waliojitokeza kuomba ridhaa ya chama kwenye Uwakilishi, Ubunge na Udiwani Zanzibar ni zaidi ya 2,098 wakati ACT hawazidi 300, watajifananishaje na sisi..?" Alihoji Mbeto.
Mwenezi huyo alibainisha kuwa hakuna jimbo hata moja ACT, wamejitokeza watu zaidi
No comments
Post a Comment