Zinazobamba

RC CHALAMILA AMEMUAGIZA MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO KUPELEKA FEDHA ZA KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA SARANGA.


Na Mussa Augustine.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amemuaguza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kupeleka fedha kiasi cha shilingi Milioni Mia Moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Saranga.

RC Chalamila ametoa agizo hilo leo April ,9,2025 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo nakuzungumza na Wananchi wa Kata ya Saranga ili kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hao,ambapo wananchi hao wamemuomba Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam kuwasidia kukamilisha haraka ujenzi huo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa baada ya kuwasikiliza wananchi hao ambao wamedai kuwa wamekua wakipata changamoto mbalimbali ya kupata huduma za  matibabu kutokana na kukosa kituo cha afya kwa muda mrefu. 

Hata hivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo amesema kuwa atatekeleza agizao hilo nakuahidi kuwasilisha fedha hizo wiki ijayo siku ya jumatano April.16,2025 ili kukamilisha ujenzi huo.

Katika hatua nyingine RC Albert Chalamila amewasihi wananchi wa Mtaa wa  Saranga kuwa wavumilivu wakati Serikali ikichukua hatua ya kutatua kero ya barabara ambayo imekua ya muda mrefu. 

Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo RC.Chalamila ametembelea Mradi wa kusukima Maji kibamba,kukagua na kuweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Mpiji Magoe,kukagua ujenzi  shule ya Sekondari Goba  kulangwa,nakuhitimisha ziara hiyo kwa  kuzungumza na kusikiliza kero za Wananchi katika Mtaa wa Saranga.

No comments