Zinazobamba

NITAHAKIKISHA KATA YA BUYUNI IMEKUA NA MAENDELEO MAKUBWA:MHE.JESCA


Diwani wa kata ya Buyuni Mhe Jesca Meckson Motto(katikati waliosimama mbele)akila kiapo wakati wa kuapishwa,hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karemjee Jijini Dar es salaam.

Na Musaa Augustine.

Diwani wa kata ya Buyuni Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe.Jesca Meckson Motto amesema kuwa kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi atahakikisha anashirikiana Vyema na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Nurdin Bilal Juma(Sheta) na Naibu wake Jonh Ryoba Mrema pamoja na watendaji wa Halmashauri ya jiji hilo katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa kata ya  Buyuni.

Amesema hayo leo Desemba 4,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuapishwa rasmi,huku akiahidi kutatua kero mbalimbali zinazowakumba Wananchi wa Buyuni ikiwemo miundombinu ya Barabaraa,Elimu,Afya Maji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii.
             Diwani Jesca Meckson Motto 
"Ndugu zangu Waandishi wa habari,leo tumemchagua Mstahiki Meya(Nurdin Bilal Juma) na naibu wake(Jonh Ryoba Mrema),pia sisi madiwani tumeapishwa rasmi ikiwa ni hatua ya kuanza kushiriki katika Baraza  la Madiwani kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo"amesema Mh.Jesca kwa bashasha kubwa.

Nakuongeza kuwa"Wananchi wa kata ya Buyuni hawajakosea kunichagua kuwa diwani wao,nimejipanga vizuri kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali za kata yetu,natamani kata ya Buyuni iwe na maendeleo makubwa,na hivyo mimi kama diwani nitahakikisha malengo hayo yanafanikiwa".



No comments