ASKARI 35 WA JESHI LA ZIMA MOTO WAPATA MAFUNZO KUTOKA TIKA UTURUKi.
Kwa msaada wa Shirika la Tika Tanzania Askari 35 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania wamepatiwa mafunzo ya msingi ya uzimaji moto na mafunzo ya msingi ya uokoaji wa mijini.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa katika hafla ya kufunga mafunzo hayo leo Aprili 17, 2025 iliyofanyika katika Ofisi za Jeshi hilo Ilala jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tika Tanzania na Mratibu wa Mafunzo hayo Firiz Sahinci amesema mafunzo hayo yamafanyika kwa siku 10 kuanzia Aprili 7 hadi Aprili 17 mwaka huu.
Feriz amebeinisha kuwa mafunzo hayo yaliongozwa na Wataalam kutoka Idara ya Zimamoto ya Manispaa ya Konya ya nchini Uturuki ambapo amesema mafunzo haya ni ya awamu ya kwanza na awamu ya pili yatafanyika Manispaa ya Konya nchini Uturuki.
Kwamba watachukuliwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania na kupelekwa nchini Uturuki, Manispaa ya Konya kwa ajili ya mafunzo ya juu zaidi ambayo yatasaidia katika kuiweka jamii salama zaidi dhidi ya majanga.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania (CGF) John Masunga amesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi katika kukabiliana na majanga ya moto na kujiimarisha kimbinu katika uokoaji

"Mpango huu ni hatua muhimu katika kujenga uwezo wa Askari wetu wa Zimamoto, koboresha mwitikio wa dharura na kuhakikisha jamii salama zaidi kwa Watanzania wote," amesema CGF Masunga.
Amebainisha kuwa mafunzo hayataishia tu kufanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam, bali wana mpango wa kuhakikisha yanafanyika na kuwafikia Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania katika mikoa yote nchini.
Amebainisha kuwa hii ilikuwa ni awamu ya kwanza ya mafunzo na kwamba katika awamu ya pili Askari 10 watakwenda Manispaa ya Konya nchini Uturuki kwa ajili ya mafunzo ya juu zaidi.
Kwamba Askari hao watakaporejea mafunzoni wataweza kuwafundisha wenzao na kuwaongezea ujuzi zaidi kwa lengo la kuboresha huduma za Jeshi hilo.
Naye Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bekir Gezer ameahidi Nchi ya Uturuki kuendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali kwani mataifa haya ni ndugu kwa muda mrefu.
Hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo hayo imeenda sambamba na utoaji wa vyeti kwa Askari wote walioshiriki mafunzo hayo.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni