Ushiriki wa NLD Katika Uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Madini
Chama cha National League for Democracy (NLD) kinapenda kuwajulisha wanachama na umma kwa ujumla kuwa Mhe. Doyo Hassan Doyo, Katibu Mkuu wa NLD Taifa, leo tarehe 2 Mei 2025, amepata fursa ya kuhudhuria kikao maalum cha uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mhe. Doyo Hassan Doyo alipata mualiko rasmi kutoka Wizara ya Madini, akihudhuria kama mmoja wa wadau wakuu wa sekta ya uchimbaji madini hapa nchini. Ushiriki huu unaonesha kwa vitendo dhamira ya NLD katika kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kusimamia, kukuza, na kuimarisha sekta ya madini kwa manufaa ya Watanzania wote.
Chama cha NLD kinaendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma, binafsi, na vyama vya siasa katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa kupitia usimamizi bora wa rasilimali za taifa.
Post Comment
No comments
Post a Comment