WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOWAZUNGUKA
Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Charangwa Seleman amewasihi wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazojitokeza ili kufikia malengo wanayotamani.
Ametoa nasaha hizo leo Mach,8,2025 kwenye Kongamano la wanawake lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam ,ambapo limeandaliwa na Taasisi ya Mwanamke na Mafanikio ( MNM) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani itakayoadhimishwa Mach 8, 2025.
Amesema kwamba wanawake wana uwezo mkubwa wa kuwa viongozi na kumiliki uchumi hivyo wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo,nakuachana na tabia za kulalamika kwani zinawapotezea muda badala ya kujikita kutafuta kipato.
"Nawaomba muwe na kiu ya kutafuta mafanikio ya malengo mnayoyatamani ,hakuna mtu atakayekuletea mafanikio nyumbani kwako ,bali mafanikio inapaswa kuyatafuta mwenyewe,wekezeni muda wenu katika kutafuta mafanikio ya maisha yenu na kutimiza ndoto zenu"...amewambia wanawake walioshiriki Kongamano hilo.
Aidha ameongeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewafungulia njia wanawake katika suala la uongozi wa ngazi za juu, hivyo wanapaswa kujivunia kuwa wanaweza kuwa viongozi katika ngazi zozote za maamuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Mafanikio ,Maria Edrick Mapunda amesema kwamba Kongamano hilo limefanyika ili kuwasidia wanawake kujitambua na kujua umuhimu wa kuchangamkia fursa zinazowazunguka.
Aidha ameongeza kuwa kongamano hilo pia linawahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaofanyika mwezi Oktoba Mwaka huu.
" Kongamano hili tumeleiandaa ili kuwakutanisha wanawake na kujadili kwa pamoja namna ya kuchangamkia fursa za uongozi,pamoja na zile zakiuchumi ili waweze kufikia ndoto zao."amesema Maria
Nakuongeza kuwa " hili Kongamano pia linawahamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaofanyika Mwaka huu ili kuweza kupata wanawake wengi kwenye vyombo mbalimbali vya maamuzi".
Baadhi ya wanawake waliohudhuria Kongamano hilo wameipongeza Taasisi hiyo kwa kuandaa Kongamano hilo kwani limewafanya kupata ujasili wa hali ya juu katika kupambania fursa mbalimbali zikiwemo za uongozi na uchumi.
Siku ya wanawake Duniani inafanyika Mach 8 kila Mwaka ,ambapo Mwaka huu imebeba kauli mbiyu isemayo"Siku ya wanawake Duniani 2025,tuongeze haki,usawa na uwezeshaji"
WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOWAZUNGUKA
Reviewed by mashala
on
12:37:00
Rating: 5
Reviewed by mashala
on
12:37:00
Rating: 5




No comments
Post a Comment