CCM:Jussa katafute jingine la Bandari limekwisha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema mchakato wa uwekezaji katika Bandari ya Malindi kisiwani Unguja umezingatia na kufuata vigezo ,sifa na taratibu za kisheria hadi kupatikana Kampuni ya Africa Global Logistic (AGL)
Pia CCM kimesisitiza hili la Bandari limekwisha hivyo kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo , Ismail Jussa Ladhu, akatafute jengine ambalo pia atajibiwa wakati wowote .
Ufafanuzi huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis, aliyesema maelezo ya Jussa yaliodai kampuni iliopewa uwekezaji sio ilioahidiwa na Serikali ni uongo na upotoshaji.
Mbeto alisema kabla ya kupatikana Muwekezaji Kampuni ya Africa Global Logistic (AGL), ulifanyika mchakato chini ya timu ya majadiliano ya SMZ uliojumuisha Kampuni kadhaa zilizoomba kutoa huduma katika Bandari ya Malindi.
Aidha alisema AGL ni kampuni ilioidhinishwa na kupiitishwa na timu ya majadiliano ya SMZ baada ya kufanyika majadiliano ya miezi 24 hadi kujiridhisha.
Baadhi ya Kampuni zilizo omba kuwekeza katika Bandari ya Malindi ni DP WORLD , ya Dubai, OIA ya Oman , AD Port ya Abudhabi na AGL ambapo tatu kati ya hizo, zilishindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na timu ya majadiliano ya Serikali
Kampuni tatu ikiwemo DP World ilitaka kutoa asilimia 13 na serikali isifanye uendelezaji wa Bandari za Wete, Wesha , Mangapwani na Fumba, hivyo upande wa Serikali haukuafiki jambo hilo .
Kampuni ya OIA ya Oman ilitaka kutoa asilimia 10, AD Port ya Abu Dhabi asilimia 9 na AGL asilimia 30, ikiwemo na uwekaji wa Teknologia ya Mifumo ya utoaji huduma za mizigo Bandarini kwa haraka.
AGL ni akampuni tanzu ya Kimataifa ya Mediterranean Shiping Company (MSC) yenye sifa za utoaji huduma za Bandari ikiwa na uzoefu mkubwa duniani.
Pia kampuni ya AGL imekuwa ikitoa huduma zake katika Bandari huko Togo, Sieralione, Liberia, Ghana,Guinea na Ivory Coast .
Nchi nyine ambazo AGL zinatoa huduma ni Comoro, Gabon, Benin Cameroon , Nigeria , Senegal na Congo .
"Jussa tunajua yuko katika juhudi akitaka ACT kionekane kipo hai mbele ya wananchi . Hakitapa turufu ya kukubalika kwa ajenda za kutunga .Hili la Bandari mwambieni limekwisha akatafute jengine' Alisema Mbeto
Hata hivyo Ka tibu huyo Mwenezi alimkanya Jussa na kumtaka aache kutumia vibaya uhuru na demokrasia ya vyama vingi kwa kupandikiza hasama na chuki katika jamii.
"Mantiki ya demokrasia katika nchi yeyote lazima ikuze ustawi wa maisha bora na kuleta maendeleo . Wananchi hawali na kushiba maneno kwenye mikutano ya hadhara. Serikali inapochukua juhudi za kuleta maendeleo ni ajabu unapomsikia mtu akileta porojo " Alieleza Mbeto
Hakuna maoni
Chapisha Maoni