Zinazobamba

*TAMASHA KUBWA LA KUMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTUNUKIWA TUZO YA GLOBAL GOAL KEEPER AWARD*

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania chini ya Mwenyekiti wake *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* unatarajia kufanya Tamasha Kubwa la Kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kutunukiwa Tuzo ya Global Goal Keeper Award Tarehe 27 Februari, 2025  katika Viwanja vya Urithi Mkoani Tanga.

*Aidha,* Tamasha hilo litaambatana na Shughuli za Huduma za Afya kama vile:-

_Upimaji wa Afya_

_Uchangiaji Damu_

_Elimu ya Uzazi Salama_

_Ushauri Nasaha_

_Msaada wa Kisheria_

*WATU WOTE MNAKARIBISHWA*

#UWTImara

#ChamaImara

#KaziIendelee

Hakuna maoni