Zinazobamba

SHIGONGO AMSHUKURU DKT.SAMIA KUPELEKA BILIONI 63 ZA MAENDLEO.

Awasihi Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt.Samia

Asema Buchosa Mpya inawezekana endapo Wananchi watashirikiana na Serikali.

Na Mussa Augustine

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Shigongo Eric James amewasihi Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazozifanya za kuwaletea wananchi Maendeleo.

Pia pamoja na mambo mengine Mbunge huyo amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kupeleka fedha kiasi cha shilingi bilioni 63 jimboni humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyokua haijatekelezwa kwa muda mrefu.

Hayo ameyasema leo Februari 22,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari,nakubainisha  kwamba nchi ya Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi ukilinganisha na nchi jirani  za Afrika Mashariki.

" Dkt Samia ameachiwa nchi na mtangulizi wake Hayyati Dkt.Jonh Magufuli ikiwa na miradi mingi ya kimkakati(SGR,Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere) ,ambayo ilikua haijakamilika,pia ilikua ni kipindi cha mripuko wa COVID-19,lakini amefanikiwa kuiendeleza miradi hiyo na hadi sasa ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji"amesema Shigongo 

Aidha amesema kuwa kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimeshuka kiuchumi kutokana na uwepo wa vita za urusi na Ukraine,pamoja na Mashariki ya kati lakini pamoja na vita hivyo Tanzania inaendelea vizuri katika kukuza uchumi wake.

Amesema kwamba sekta ya Utalii,Kilimo,Madini zinazidi kukukua nakuchangia pato kubwa kwa Taifa nakwamba inapaswa kuheshimu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwaletea wananchi Maendeleo.
Akizungumzia kuhusu Maendeleo katika Jimbo la Buchosa Mh.Shigingo amesema kwamba anamshukuru  Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha zaidi ya bilioni 62.3 ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake,nakwamba jimbo lake la Buchosa kwa sasa limepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu ya  Barabara,Maji,Afya na Elimu.

"Namshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,na chama changu cha CCM kwa ujumla,tumejenga barabara,Vituo vitano(5) vya afya,sekondari mpya nane(8),zahanati ishirini  na moja(21), Madarasa yakutoshereza kila kona,hivyo sina budi  kumshukuru Rais Dkt Samia kwa kutuletea fedha hizo kwa ajili ya maendeleo kwa Wananchi wa Buchosa".

Hata hivyo katika hatua nyingine amesema kwamba fedha za Maendeleo zinazotolewa na Serikali kwenye majimbo zimekua zikisimamiwa vizuri katika utekelezaji wake ndio maana vitendo vya ubadhilifu wa fedha za miradi kwa sasa nchini vimepungua.

"Wanaoendelea kufanya ubadhilifu wa fedha za umma wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo"amesema

Nakusisitiza kuwa"haiwezekani Rais Dkt Samia atafute fedha za Maendeleo Nchini halafu wachache wasiokua na uchungu na maendeleo ya wananchi,wazitafune fedha hizo halafu wasichukuliwe  hatua":


Hakuna maoni