Zinazobamba

Mbeto atabiri ACT kusambaratika Zbar

Mwandishi  Wetu , Zanzibarh

Chama Cha Mapinduzi  (CCM) kimetabiri  licha  ya ACT  Wazalendo kuwa kitashindwa Uchaguzi Mkuu Oktoba  Mwaka huu,  kuna dalili  zote za kufa  mikononi mwa uongozi wa  Mwenyekiti  Othman Masoud  Othman na Makamu wake, Ismail Jussa Ladhu .

Hakiwezi  kufika popote  baada ya  idadi kubwa ya wanachama wa ACT  kuchoshwa na uongozi wa kidikteta na kebehi za Jussa.

Hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar,  Idara  ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto  Khamisi  , aliyedai  kuna  dalili ya  ACT kufikwa kwa  mwisho  mbaya wa uongozi   chini  ya viongozi hao wawili.

Mbeto  alisema ikiwa baadhi ya wanachama waasis na vigogo wa   ACT  katika ngazi mbalimbali wanakilalamikia chama chao kuendeshwa kidikteta ,dharau na kiburi, chama hicho kinaweza kukatika na kufa  .

Alisema  kuna wanachama ambao wameanza kuhoji kwanini  Othman  apewe uongozi wa juu wakati alikataa  kukiunga mkono CUF  na kutoshriki  harakati za upinzani na wakati  wote   alikuwa mtumishi mtiifu SMZ .

"Jussa na Othman kaeni kwa makini  chama kitawafia mikononi mwenu.  Historia ya ACT itawaandika kwa wino  wa  machozi ya aibu. Hamtakiwi ndani ya ACT  anzeni kujitafakari upya "Alisema Mbeto. 

Aidha  Katibu huyo Mwenezi,  alisema  kikundi cha watu saba  ndani ya  ACT ambao ndio wanaopitisha maamuzi yote  kuliko  katiba ya ACT,  baadhi ya wanachama  wanapinga aina ya uongozi usiozingatia maamuzi ya pamoja  . 

"Kuna wanachama wengi  wanataka kurudi  CUF . Madai yao hawamtaki Jussa  .Wanahoji  alikopata utajiri  wakati hana kazi wala biashara  .Othman  ajipime kama unatosha ili  asifikwe na fedheha kwa dhambi  za Jussa " Alisisitiza 

Mbeto  alidai  tokea Mwaka 1992 ,Othman  aliitwa na Hayati  Maalim  Seif Sharif Hamad  ili akiunge mkono CUF  akakataa hivyo hakuna sababu  yoyote ya kupewa madaraka ya juu ACT. 

"Madai ya Jussa  kusema Othman alipendekezwa toka  wakati  wa uhai wa  hayati  Maalim seif  , ni hadithi ya kutunga na  uongo . Haiwezekani Maalim Seif amtaje Othman na kuwaacha kina  Juma Duni au  Mohamed  Dedes " Alieleza

Hata hivyo  baadhi ya wanachama wa ACT  wamekasirishwa na uamuzi  wa kikundi  cha watu saba  ACT kuanza kumpigia debe  la kugombea urais wa Zanzibar   Othman   kabla  ya kufanyika maamuzi ya vikao vya kikatiba

Hakuna maoni